Tuesday, September 24, 2013

HALMASHAURI YA WILAYA YA BUSOKELO YAKABIDHIWA GARI NA WIZARA YA AFYA

Mganga Mkuu wa Serikali Dk. Donan Mmbando akielezea hali ya huduma za chanjo nchini  katika hafla fupi ya kukabidhi gari   aina ya ‘Toyota double Cabin’ kwa ajili  ya huduma ya chanjo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo lenye thamani ya  Sh. milioni 38  iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara ya  Afya na Ustawi wa Jamii jijini Dares Salaam leo. 2 
Katibu Mkuu wa Wizara  ya Afya na Ustawi wa Jamii,Charles Pallangyo akizungumzia na waandishi wa habari leo katika hafla fupi ya kukabidhi gari   aina ya ‘Toyota double Cabin’ kwa ajili  ya huduma ya chanjo kwa Halimashauri ya Wilaya ya Busokelo lenye thamani ya  Sh. milioni 38  jijini Dares Salaam leo.Kulia ni Waziri  wa  nchi  Ofisi ya Rais (Kazi maalumu), Profesa Mark Mwandosya. 3Mwenyekiti wa halimashauri hiyo,Meckson Mwakipunga(aliyesimama) akiishukuru Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa msaada wa gari hilo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Rungwe,Crispin Meelana kulia ni Mganga Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Dk. Gilibert Tarimo 4 5Mwenyekiti wa halimashauri hiyo,Meckson Mwakipunga akijaribu kuendesha gari walilopewa na Wizara ya Afya naUstawi wa Jamii leo jijini Dares Salaam. 6 
Waziri  wa  nchi  Ofisi ya Rais (Kazi maalumu), Profesa Mark Mwandosya(kulia) akijadiliana jambo na baadhi ya watu wakati  hafla fupi ya kukabidhi gari   aina ya ‘Toyota double Cabin’ kwa ajili  ya huduma ya chanjo kwa Halimashauri ya Wilaya ya Busokelo lenye thamani ya  Sh. milioni 38  jijini Dares Salaam leo. 7  
Waziri  wa  nchi  Ofisi ya Rais (Kazi maalumu), Profesa Mark Mwandosya wa pili (kulia mbele) akiwa katika picha ya pamoja na  baadhi ya watu wakati  hafla fupi ya kukabidhi gari   aina ya ‘Toyota double Cabin’ kwa ajili  ya huduma ya chanjo kwa Halimashauri ya Wilaya ya Busokelo lenye thamani ya  Sh. milioni 38  jijini Dares Salaam leo.
Picha zote na Magreth Kinabo –MAELEZO.
......................................................
 

WAZIRI PROFESA MWANDOSYA ASEMA SERIKALI INAFANYA MENGI WENYE MACHO WANAONA

Mwandosya-Mark
Profesa Mark Mwandosya

NA   MAGRETH KINABO- MAELEZO
 
WAZIRI   wa  nchi  Ofisi ya Rais (Kazi maalumu), Profesa Mark Mwandosya amesemwa Tanzania itafikia maendeleo ya hali ya juu ifikapo mwaka 2025 hadi mwaka 2030 ikiwa watu watafanyakazi kwa upendo, uzalendo na kujiamini.
 
Aidha Profesa Mwandosya amesema kwamba Serikali inajitahidi kufikisha huduma zake kwa  karibu na wananchi, licha ya kuwepo kwa changamoto za kielimu na miundombinu, lakini mambo mengi yanafanyika,hivyo wenye macho wanaona.

Kauli hiyo imetolewa leo na  Profesa Mwandosya wakati hafla fupi ya  kukabidhi gari  aina ya ‘Toyota double Cabin’ kwa ajili  ya huduma ya chanjo kwa Halimashauri ya Wilaya ya Busokelo lenye thamani ya  Sh. milioni 38  iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara ya  Afya na Ustawi wa Jamii jijini Dares Salaam.
 
“ Mimi nina matumaini makubwa  na nchi yetu ifikapo mwaka 2025 hadi 2030 tutakuwa ni nchi yenye watu wenye kipato cha kati.Pia ifikapo mwaka 2050 nchi yetu itakuwa imeendelea hakutakuwa na mtu mwenye kipato cha kati wala cha chini kama ilivyo nchi ya Singapore,” alisema Profesa Mwandosya.
 
Profesa Mwandosya aliongeza kuwa  gari hilo ni moja ya juhudi za Serikali za kuhakikisha kuwa huduma  zake zinaifikia jamii  kila mahali hususan  kwenye maeneo ya vijijini.
“Serikali inajitahidi kufikisha huduma zake mfano katika sekta ya elimu kuna mambo mengi yamefanyika na yanaendelea kufanyika ikiwemo katika sekta nyingi kama vile kwenye nishati  gesi  tunakwenda vizuri.  Tukisimamia vizuri rasilimali zetu ,basi   hata  huduma tutazifikisha vizuri kwa wananchi,” alisisitiza.
 
 “ Kila mtu duniani anasema Tanzania inapiga kasi  katika kuwaletea maendeleo  wananchi . Mimi  nadhani hatutarudi nyuma. Wale wanaopiga kelele hautajafanya kitu ,lakini mwenye macho wanaona,” alisisitiza Profesa Mwandosya.
 
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Charles Pallangyo akizungumzia kuhusu gari hilo alisema litasaidia kuhimarisha huduma za chanjo katika halimashauri hiyo na kupunguza vifo vya wakinamama wajawazito na watotowenye umri wa chini ya miaka mitano ili kutimiza malengo ya millinea ya namba 4na 5 ifikapo mwaka 2015.
 
 Naye Mganga Mkuu wa Serikali Dk. Donan Mmbando alisema nchi hivi sasa imefikia wastani wa asilimia 92 katika huduma za chanjo kutoka asilimia 90 ya kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
 
Mwenyekiti wa halimashauri hiyo,Meckson Mwakipunga aliishukuru wizara hiyo kwa msaada huo ,ambapo alisema gari hilo litatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuinua kiwango cha huduma hiyo kwenye eneo hilo.

No comments: