Sunday, September 22, 2013

RAIS KIKWETE ATUNUKIWA SHAHADA YA UZAMIVU YA CHUO KIKUU CHA GUELPH JIMBONI ONTARIO, CANADA


Sehemu ya umati ulioshuhudia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kutunukiwa Shahada  ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20, 2013
t9 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitunukiwa Shahada ya Uzamivu na Provost na Makamu wa Rais wa  Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario, Dkt Maureen Mancuso  , Ijumaa Septemba 20, 2013 t10 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akishangiliwa katika  Chuo Kikuu Guelph baada ya kutunukiwa Shahada  ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20, 2013 Ijumaa Septemba 20, 2013. t11 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia  Chuo Kikuu Guelph baada ya kutunukiwa Shahada  ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20, 2013 t12Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Guelph pamoja na na  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa  na  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe baada ya kutunukiwa Shahada  ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20, 2013 Ijumaa Septemba 20, 2013 t13 
Umati ulioshuhudia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kutunukiwa Shahada  ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20, 2013 t15 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Wakuu wa Chuo Kikuu Guelph pamoja na na  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa  na  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe baada ya kutunukiwa Shahada  ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20, 2013  Ijumaa Septemba 20, 2013
t16 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa baada ya kutunukiwa Shahada  ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20, 2013 t17 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa (kulia) na  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe baada ya kutunukiwa Shahada  ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20, 2013
PICHA NA IKULU

……………
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete  Ijumaa, Septemba 20, 2013, ametunukiwa Shahada ya Uzamivu (PHD) na Chuo Kikuu cha Guelph katika jimbo la Ontario nchini Canada kwa kutambua mchango na uongozi wake katika kuleta mageuzi ya kilimo katika Afrika.   
Viongozi wa Chuo hicho wanasema kuwa wamefanya uamuzi wa kumtunuku Rais Kikwete kutokana na jitihada zake za kukabiliana na changamoto zinazokabili kilimo, jitihada zake za kuleta usalama wa chakula na pia majaribio makubwa ya kuongeza matumizi ya technolojia katika kilimo cha Tanzania na Afrika.
  Rais Kikwete ambaye amewasili Canada usiku wa Alhamisi, Septemba 19, 2013 akitokea Washington, D.C., Marekani ambako alikuwa kwa siku mbili akitokea Jimbo la California amekuwa Mtanzania wa kwanza kutunukiwa shahada ya juu kabisa katika historia ya Chuo hicho.
Chuo cha Guelph ni moja ya vyuo vikuu vinavyoheshimiwa zaidi katika Canada na duniani katika Nyanja za kilimo na kilianzishwa rasmi kama Chuo cha Kilimo cha Jimbo la Ontario Mei Mosi, mwaka 1874.
 Chuo hicho ambacho kimejipatia umaarufu kutokana na ubora wa shughuli zake za utafiti kimekuwa katika mstari wa mbele kutafuta majawabu ya changamoto zinazoikabili dunia katika masuala ya kilimo, raslimali za maji, matatizo makubwa ya magonjwa ya mimea, matatizo ya ukuaji haraka wa miji duniani na changamoto za biashara za kimataifa.
 Katika miaka ya karibuni kufuatia tishio kubwa kimataifa la ongezeko la bei za vyakula duniani na hasa katika nchi masikini, mabadiliko ya tabianchi, ongezeko la uchafuzi wa hali ya hewa, uharibifu wa mazingira, changamoto za upatikanaji wa maji safi na salama duniani, kazi ya Chuo hicho imeongezeka sana.

Chuo hicho kimeichagua Tanzania kama nchi ya kufanya nayo kazi katika Afrika kukabiliana na changamoto hizo na kimemtambua Rais Kikwete kutokana na mchango wake mkubwa katika sekta ya kilimo katika miaka yote ya uongozi wake na mipango yake ya kuboresha kilimo katika Tanzania kama ASDP, Kilimo Kwanza na SAGCOT ambayo yote inasifiwa sana kimataifa.
Chuo hicho kina mahusiano ya karibu na Vyuo Vikuu vya Dar es Salaam, Sokoine cha Mzumbe – Morogoro na UDOM – Dodoma. Kati ya mwaka jana na mwaka huu, Chuo hicho kimetiliana saini Makubaliano ya Ushirikiano (MOU) na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine cha Mzumbe – Morogoro na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Mara nne kati ya Januari, mwaka jana, 2012 na Juni, mwaka huu, 2013, uongozi wa Chuo hicho ukiongozwa na Rais na Makamu Mkuu wa Chuo, Dkt. Alastair Summerlee na Makamu wa Rais wa Utafiti Dkt. Kevin Hall umetembelea Tanzania na kukutana na viongozi wa Serikali pamoja na wale wa Vyuo Vikuu vya Dar Es Salaam na Sokoine cha Mzumbe, Morogoro.
            Mbali na ujumbe ambao unaongozana na Rais Kikwete, sherehe za kutunukiwa kwa Kiongozi Mkuu huyo wa Tanzania pia zimehudhuriwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe, Jumuia ya Watanzania wanaoishi Canada pamoja na maofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini humo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
20 Septemba, 2013

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

DSC00382 
“PRESS RELEASE” TAREHE 21. 09. 2013.
WILAYA YA RUNGWE – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU
NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 20.09.2013 MAJIRA YA SAA 12:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA NDAGA WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. GARI T.565 AINA YA TOYOTA COASTER  LIKIENDESHWA NA  DEREVA SHABAN S/O IDDI, MIAKA 32, MKINGA, MKAZI WA TUKUYU  LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MTOTO  KALEBO S/O EZEKIA,  MIAKA 5, KYUSA,  MKAZI WA KIJIJI CHA  NDAGA NA KUSABABISHA KIFO PAPO HAPO.  CHANZO MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. DEREVA AMEKAMATWA, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. 

WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO]
MNAMO TAREHE 20.09.2013 MAJIRA YA SAA 15:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MBANGALA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA.  ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA PAUL S/O MAHAGA  MIAKA 22, MSUKUMA, MKULIMA, MKAZI WA MBANGALA   AKIWA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA TATU [03]. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA  WITO KWA  JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA  MOSHI [GONGO]  KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.
Signed by:
                                                      [DIWANI ATHUMANI - ACP]
                                         KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments: