Thursday, September 26, 2013

MAGARI MANNE YAGONGANA NA KUSABABISHA VIFO MBEYA          WILAYA YA MBEYA VIJIJINI - AJALI YA MAGARI MANNE KUGONGANA NA
                                                              KUSABABISHA VIFO.  
§  MNAMO TAREHE 26.09.2013 MAJIRA YA SAA 06:45HRS HUKO KATIKA MTEREMKO WA PIPE LINE INYALA BARABARA YA MBEYA/IRINGA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. GARI T.605 AXX /T.480 CAX AINA YA  SCANIA LORI LIKITOKEA NCHINI ZAMBIA KUELEKEA DAR – ES SALAAM LIKIENDESHWA NA DEREVA WILSON  MACHA, AKIWA NA TINGO WAKE JUMA S/O SALEHE WOTE WAKAZI WA DSM [AMBAO KATIKA AJALI HIYO WOTE WAMEFARIKI DUNIA] LILIGONGA KWA NYUMA GARI T.548 BLY/ T.974 BVN AINA YA  SCANIA LORI LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA SAMWEL  ARON, MIAKA 30, MBENA, MKAZI WA SINZA, KISHA GARI HILO LILILIGONGA GARI T.876 BKV/T.465 BQU AINA YA  IVECO LORI AMBALO LILIKUWA LIMEEGESHWA PEMBENI YA  BARABARA LIKIWA LIMEHARIBIKA, LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA SAMWEL  KASUSU, MIAKA 37, MJITA, MKAZI WA GONGO LA MBOTO DSM.
§  AIDHA GARI HILO  T.605 AXX /T.480 CAX LIKIWA LIMEPOTEZA MWELEKEO LILIGONGANA USO KWA USO NA GARI T.255 AKV/T.272 CDZ AINA YA  SCANIA LORI LILILOKUWA LIKITOKEA DSM KUELEKEA MBEYA MJINI AMBALO LILIKUWA LINAENDESHWA NA DEREVA SIXTUS S/O KAPINGA, MIAKA 35,MNGONI, MKAZI WA DSM AMBAYE ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO NA MWILI WAKE KUTEKETEA KWA KUUNGUA MOTO.
§   KATIKA AJALI HIYO  MAGARI MAWILI T.605 AXX /T.480 CAX  NA  T.255 AKV/T.272 CDZ  YOTE YAMEUNGUA VICHWA NA KUTEKETEA NA GARI  T.548 BLY/ T.974 BVN LILIUNGUA KIDOGO SEHEMU YA  KICHWA UPANDE WA KULIA.
§  CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA GARI T.605 AXX /T.480 CAX.
§  MOTO ULIZIMWA KWA USHIRIKIANO KATI YA KIKOSI CHA ZIMA MOTO NA UOKOAJI KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI NA WANANCHI.
§  MIILI YA MAREHEMU WILSON  MACHA NA JUMA  SALEHE IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. JITIHADA ZA KUUTOA  KATIKA GARI MWILI WA MAREHEMU  SIXTUS S/O KAPINGA PAMOJA NA KUTOA MAGARI ENEO LA TUKIO  ZINAENDELEA.  
§   KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA  ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Signed By:
                                                      [DIWANI ATHUMANI - ACP]
                                         KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
    PICHA NA MDAU
Post a Comment