Thursday, September 26, 2013

WATUHUMIWA 34 WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA KULA NJAMA NA KUFANYA FUJO/KUFUNGA BARABARA KUU MBEYA /TUKUYU


WATUHUMIWA WAKISHUSHWA KWENYE GARI KUINGIZWA MAHAKAMANI KUSOMEWA MASHITAKA YAO
WATUHUMIWA WAKIPATA CHAI MAHAKAMANI HAPO
HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA SIKU MGOMO WA WAKULIMA HAKUNA KILICHOUZWAWILAYA YA RUNGWE -   WATUHUMIWA 34 WAMEFIKISHWA                                                    
                                                                                  MAHAKAMANI TAREHE
                                                                                  25.09.2013 NA JESHI LA
                                                                                  POLISI KWA KOSA LA KULA NJAMA
                                                                                  NA KUFANYA FUJO/KUFUNGA
                                                                                  BARABARA KUU MBEYA/TUKUYU KWA
                                                                                  MAWE NA MAGOGO.
                                                   
§  MNAMO TAREHE 25.09.2013 MAJIRA YA  SAA 15:35HRS HUKO KATIKA MAHAKAMA YA  WILAYA ILIYOPO  - TUKUYU MJINI WILAYA YA  RUNGWE MKOA WA MBEYA. LAURENT S/O NICHOLAUS KASWAGA, MIAKA 38, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA IBURA – KIWIRA NA WENZAKE 33 WALIFIKISHWA KATIKA MAHAKAMA YA  WILAYA NA KUSOMEWA MASHTAKA MAWILI 1. KULA NJAMA NA 2. KUFANYA FUJO. AIDHA WATUHUMIWA WALISOMEWA MASHTAKA HAYO NA MWENDESHA MASHTAKA WA POLISI F.3644 D/C JOEL  MBELE YA  HAKIMU WA MAHAKAMA HIYO MHE. MEBO MALAKASUKA.
§  KATIKA SHAURI HILO LA JINAI NO. 169/2013 WASHTAKIWA WOTE WAMEPELEKWA GEREZANI AMBAPO UAMUZI WA KUPEWA AU KUTOPEWA DHAMANA UTATOLEWA NA MAHAKAMA  TAREHE   09.10.2013.
§  AWALI MNAMO TAREHE 24.09.2013 MAJIRA KATI YA  SAA 18:00HRS HADI SAA 22:00HRS HUKO KATIKA KATA YA  KIWIRA VITONGOJI VYA KIBUMBE, MPANDAPANDA, KIWIRA – KATI  NA KARASHA WILAYA YA  RUNGWE MKOA WA MBEYA. KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WALIFANYA FUJO KWA KUFUNGA BARABARA KUU YA  MBEYA/TUKUYU WAKITUMIA MAWE MAKUBWA NA MAGOGO ILI MAGARI YASIPITE NA KUSABABISHA USUMBUFU KWA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA HIYO. THAMANI HALISI YA  UHARIBIFU ULIOTOKEA BADO KUFAHAMIKA.
§  HATA HIVYO KATIKA TUKIO HILO GARI T.335 CBE AINA YA  TOYOTA L/CRUISER LIKITOKEA MBEYA MJINI KUELEKEA TUKUYU LIKIWA LIMEBEBA MIILI YA  MAREHEMU WATATU LILIGONGA MAWE YALIYOKUWA YAMEWEKWA BARABARANI NA WATU HAO KISHA KULIGONGA GARI T. 771 BBE AINA YA  TOYOTA COASTER NA KUSABABISHA MAJERUHI KWA WATU WAWILI  NA UHARIBIFU KWA MAGARI YOTE MAWILI. CHANZO  CHA VURUGU HIZO  NI MADAI YA  KUONGEZEWA USHURU WA MAZAO [NDIZI] KUTOKA TSHS 100/=  ULIOANZA KUTUMIKA MWAKA 1989 NA KUFIKIA TSHS 200/= WAKISHINIKIZA URUDISHWE USHURU WA ZAMANI NA KUFUATIA VURUGU HIZO JUMLA YA  WATUHUMIWA 43 WALIKAMATWA.
§   KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO  KWA JAMII KUWA CHANGAMOTO KATIKA JAMII HAZIWEZI KUTATULIWA KWA KUWEKA MAGOGO NA MAWE BARABARANI BADALA YAKE WATAFUTE UFUMBUZI KWA KUWASILISHA MATATIZO  KERO NA MAONI  YAO KATIKA MAMLAKA HUSIKA NA KUKAA  MEZA YA  MAZUNGUMZO ILI KUPATA UFUMBUZI KWA KUZINGATIA HOJA.
AIDHA ANASISISTIZA KUWA KUFUNGA BARABARA KUNALETA MADHARA KWA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA WAKIWEMO WAGONJWA, WASAFIRI, WAGENI KUTOKA MATAIFA MBALIMBALI PIA KUSAFIRISHA MAITI KAMA ILIVYOTOKEA KATIKA GARI T.335 CBE NA KWAMBA JESHI LA POLISI KAMWE HALITASITA KUWACHUKULIA HATUA ZA KISHERIA WATU /KIKUNDI CHA WATU WATAKAOSABABISHA UVUNJIFU WA  AMANI.KWA SASA HALI YA  ENEO HILO NI 
Post a Comment