Monday, September 30, 2013

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

DSC00265 
DIWANI ATHUMANI – ACP -KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
………………………………………………………………………..
“PRESS RELEASE” TAREHE 29. 09. 2013.
WILAYA YA MBARALI – MAUAJI.
MNAMO TAREHE 28.09.2013 MAJIRA YA SAA 14:00HRS HUKO UTENGULE WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. JIDAYI S/O JINGAZA, MSUKUMA,   MIAKA 26, MKULIMA, NA MKAZI WA UTENGULE ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIPATIWA MATIBABU KATIKA KITUO CHA AFYA IGURUSI BAADA YA  KUJERUHIWA KWA KUPIGWA NA FIMBO KICHWANI NA WATUHUMIWA  WANNE AMBAO NI {1} DONGEA S/O INAMBILI {2} KAMTIMBO S/O INAMBILI {3} INAMBILI S/O INAMBILI NA MTUHUMIWA MMOJA AMBAYE  BADO HAJAFAHAMIKA. CHANZO CHA MAUAJI NI UGOMVI ULITOKANA NA WATUHUMIWA KUTAKA KUMBAKA DADA WA MAREHEMU, WATUHUMIWA WAMETOROKA MARA BAADA YA TUKIO HILO JUHUDI ZA KUWATAFUTA ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI WALIPO WATUHUMIWA  WALIYOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.


WILAYA YA MBARALI – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU
NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 28.09.2013 MAJIRA YA SAA 20:45HRS HUKO MASHALA IGURUSI BARABARA YA MBEYA/IRINGA. GARI NO T.274 AUA AINA YA SUZUKI ESCUDO LIKIENDESHWA NA   DEREVA JOHN S/O MSHONGO. MIAKA 38, MPARE , DAKTARI, NA MKAZI WA FOREST MBEYA, LILIMGONGA MPANDA BAISKELI AITWAYE OBED S/O DONARD, MIAKA 32, MBENA, MKAZI WA MASHALA NA KUSABABISHA  KIFO CHAKE PAPO HAPO. MWILI WA MAREHEMU UMEKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA TARATIBU ZA MAZISHI. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI, DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA MBOZI – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU
NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 28.09.2013 MAJIRA YA SAA 13:30HRS HUKO MLOWO BARABARA YA MLOWO/KAMSAMBA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. GARI NO T.372 BYD AINA YA  T/NOAH LIKIENDESHWA NA DEREVA DAVID S/O ALEXANDER  @ MWAIPUNGU, MIAKA 30, MNYAKYUSA, MKAZI WA MLOWO LILIMNGONGA MTEMBEA KWA MIGUU AITWAYE SHUKURANI S/O MBEMBELA, MIAKA 32, MNDALI, DEREVA WA PIKIPIKI{BODABODA} NA MKAZI WA MLOWO  NA KUSABABISHA KIFO CHAKE WAKATI AKIPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA  SERIKALI VWAWA – MBOZI. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KA
MISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. 
Signed by:
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
                                         KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
........................................................
 

MISS UTALII KUITANGAZIA DUNIA KUPATIKANA KWA NYATI WA AJABU KATIKA HIFADHI NGORONGORO

NYATI MWEUPE NGORONGORO MISS TOURISM TZZ 
Miss Utalii Tanzania 2013, Hadija Said Mswaga, amesema kuwa kupatikana kwa nyati mweupe wa ajabu na pekee duniani katika hifadhi ya Ngorongoro, imekuwa ni chachu na kichocheo cha pekee kwake katika mpango mkakati wake wa kuitangaza Hifadhi ya Ngorongoro kitaifa na kimataifa, ambapo kwa kuanzia ameamua kuanza kampeni hiyo kupitia mashindano ya dunia anayokwenda kushiriki ya Miss Tourism World 2013, ambayo mwaka huu yanafanyikia nchini Equatorial Guinea Octoba 12, 2013.
Kupatikana kwa Nyati huyo wa ajabu Mweupe, ambaye hapatikani sehemu nyingine yoyote Duniani, wakati huu ambao anakwenda katika mashindano hayo ya Dunia, imekuwa ni fulsa ya pekee kwa Tanzania, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na kwake , kuithibitishia dunia kuwa Ngorongoro Cater ni Ajabu la Asili la Dunia Barani Afrika. Ambapo sasa Ngorongoro Crater  pamoja na maajabu ya bonde lenyewe la kreta ya Ngorongoro, pia kuna maajabu ya Nyati Mweupe, Unyayo wa Binadamu wa kale zaidi Duniani, Mchanga wa ajabu unao hama kila mwaka kwa umbo la Nusu mwezi, Mlima wenye Volkano Hai wa Oldonyo Lengai, lakini pia ushirikiano wa kuishi bila kudhuriana wa binadamu na Wanyama katika hifadhi hiyo na upatikanaji wa jamii karibu zote za Wanyama wakubwa (BIG FIVE) na adimu duniani wakiwemo Faru Weusi,Duma,Mbwa Mwitu, Kaka kuona n.k.
Ngorongoro Crater na Hifadhi nzima ya Ngorongoro ni tunu ya Taifa la Tanzania, nahazina ya Dunia ambayo tunapaswa kuienzi na kuitangaza kwa nguvu zetu zote, ili iweze kuingiza pato na kuchangia zaidi uchumi na pato la Taifa, lakini pia kukuza na kuendeleza huduma za jamii ,ikiwemo elimu na afya. Naupongeza uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwa jitihada zao za kukuza utalii na kupambana na majangili , nawaomba kuimarisha na kuongeza mapambano na vita dhidi ya ujangili na majangili, ili kuhakikisha kuwa majangili hao hawamdhuru nyati huyo wa ajabu na Wanyama wengine katika hifadhi hiyo. Lakini pia naiomba mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kumlinda nyati huyo dhidi ya Wanyama wengine wala nyama kama samba n.k.
Wafanyakazi wa hifadhi hiyo Ijumaa ya tarehe 27-9-2013 asubuhi wakiwa katika basi la mamlaka wakienda kazini walimshudia Nyati huyo akiwa na kundi la nyati wengine kandokando ya barabara ndani ya hifadhi hiyo. Jambo ambalo liliwavutia na dereva wa basi hilo kulazimika kusimamisha basi kutoa fulsa kwa wafanyakazi hao kumshudia nyati huyo na baadhi yao kupiga picha kwa simu zao na kamera walizokuwa nazo.
Hadija ameushukuru uongozi wa Ngorongoro , kwa kumpatia DVD zaidi ya 100 ya hifadhi hiyo,ambazo atakwenda kuzigawa kwa washiriki wote 126 na vituo vya Televisheni vya nchi zao wanaoshiriki katika mashindano hayo ya Dunia ya Miss Tourism World 2013 mwaka huu. Baada ya kurudi nitazunguka nchi nzima na dunia nzima kuitangaza Ngorongoro kwa kushirikiana na Uongozi wa Miss Tourism Tanzania Organisation na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

No comments: