Tuesday, September 10, 2013

Wanafunzi 868,030 kuhitimu Darasa la Saba

wanafunzi_92410.jpg
Wanafunzi 868,030 wa Darasa la Saba wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi Jumatano na Alhamisi wiki hii, ikiwa ni mwanzo wa mpango wa Serikali wa Matokeo Makubwa Sasa utakaotekelezwa kwa kuanzia katika mitihani hiyo. Taarifa ya Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), inaonyesha kuwa wanafunzi hao wanatoka kwenye shule 15,677 zikiwamo za umma na binafsi.


Inaeleza taarifa hiyo kuwa, wanafunzi wanaotarajiwa kufanya mtihani wa lugha ya Kiswahili ni 844,810 kati yao wasichana wakiwa 444,475 na wavulana 400,335. Kati ya wanafunzi hao, wasioona ni 88 wavulana wakiwa ni 56 na wasichana 32 huku wenye uono hafifu wakiwa 546 na kati yao wavulana ni 263 na wasichana 283.
Watakaofanya mtihani huo kwa lugha ya Kiingereza ni 22,535 na kati yao wavulana wakiwa 11,430 na wasichana 11,105. Wanafunzi wenye uono hafifu kati ya hao ni 51, wavulana wakiwa 21 na wasichana 30.

Mwaka jana wanafunzi 894,881 kutoka shule 15,363 walifanya mtihani huo, huku wale waliofanya mtihani huo kwa lugha ya Kiswahili wakiwa 873,837 wavulana walikuwa 415,572 na wasichana 458,265.
Waliofanya mtihani huo kwa lugha ya Kiingereza walikuwa 20,457 wavulana wakiwa 10,422 na wasichana 10,035. Wenye uono hafifu walikuwa ni 45 wavulana wakiwa 26 na wasichana 19.
Msemaji wa Necta, John Nchimbi, alilieleza gazeti hili kuwa tayari mitihani imeshasambazwa huku akionya kuhusu wale watakaojaribu kufanya udanganyifu wa aina yoyote ile.
"Tunawataka wanafunzi na wadau wote wanaohusika na mtihani huu, wasije wakajihusisha na udanganyifu kwa namna yoyote ile, Necta tupo makini na tumejipanga kwa chochote kitakachotokea," alisema na kuongeza:

"Tunaamini kuwa wanafunzi wameandaliwa vya kutosha na wao ni vyema wajiandae zaidi kisaikolojia, yeyote atakayebainika kufanya udanganyifu tutamchukulia hatua zinazostahili ikiwa ni pamoja na kumfutia matokeo."

Wanafunzi hawa wanaanza mtihani wakati ambapo Serikali imeweka lengo la kuinua ufaulu wa mtihani huo kutoka asilimia 31 za mwaka jana mpaka 60 mwaka huu ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa
Chanzo:Mwananchi
....................................................................

Wasimamizi wa mtihani waaswa kusimamia kwa umakini na uadilifu

Na 1-Elimu 
Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  kuhusu mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi Tanzania Bara, ambao unaotarajiwa kufanyika Septemba 11 na 12 mwaka huu. Kushoto kwake ni Naibu Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani Tanzania Dkt. Charles Msonde. Na.2-Elimu 
Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuhusu mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi Tanzania Bara, ambao unaotarajiwa kufanyika Septemba 11 na 12 mwaka huu. Kulia kwake ni Kamishina wa Elimu Tanzania Prof. Eustela Bhalalusesa, kushoto kwake ni Naibu Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani Tanzania Dkt. Charles Msonde. Na.3-Elimu 
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika kutekeleza majukumu yao katika mkutano na Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo (hayupo kwenye picha) jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumzia kuhusu mtihani wa taifa wa darasa la saba, unaotarajiwa kufanyika Septemba 11 na 12 mwaka huu.
WILAYA YA RUNGWE MKOANI MBEYA

MOJA YA MAGALI YA ZAMANI YANAYOTUMIKA HADI SASA. HILI NI GALI LA CHUO CHA UALIMU MPUGUSO NA HAPA NI MOJA LA GALI LITAKALO TUMIKA KUWASAMBAZA WASIMAMIZI WA MITIHANI KATIKA VITUO VYAO VYA KUFANYIA MITIHANI INAYOTARAJIA KUANZA KESHO

OFISI YA HALMASHAURI YA RUNGWE TUKUYU

WALIMU WA SHULE MANBALIMBALI WILAYANI RUNGWE WALIOCHAGULIWA ILI KUFANIKISHA KUFANYIKA KWA MITIHANI YA DARASA LA SABA  WAKIPATA MAELEKEZO YA MUHIMU KATIKA VIUNGA VYA HALMASHAURI YA RUNGWE MJINI TUKUYU MKOA WA MBEYA  HAPA KABLA YA KUTAWANYWA KATIKA VITUO VYA KUFANYIA MITIHANI

MWALIMU ROBART KAGALI AKIWA MMOJA WA WASIMAMIZI WA MITIHANI YA DARASA LA SABA WILAYANI RUNGWE MITIHANI INAYOTARAJIWA KUANZA KESHO

KUSHOTO MWALIMU CAROLINE NICHOLAUS  AKIWA ANAELEKEA KUPATA MAELEKEZO YA USIMAMIZI WA MITIHANI

USALAMA KWANZA ILI KUFANIKISHA USIMAMIZI MZURI WA MITIHANI
MITIHANIYADARASALASABAMORO2 fc956

SERIKALI imewataka wasimamizi watakaosimamia mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi kufanya kazi yao ya kusimamia kwa umakini na uadilifu wa hali ya juu, huku ikiwaonya wale watakaokiuka agizo hilo kuwa watachukulia hatua za kisheria.
 
Post a Comment