Tuesday, October 29, 2013

BABA NA SHANGAZI WAENDELEA VYEMA, MUNGU NI MWEMA, LAKIN MIAKA ZAIDI YA SABA BABA RAJABU KINGO ANASUBIRI MAFAO YAKE YA USTAFU TAZARA

NIPO NA BABA MKUBWA WANGU  MZEE RAJABU KINGO TUMEONGEA MENGI SANA KWA SASA ANGALAU BABA ANENDELEA VYEMA NA AFYA. BABA MKUBWA RAJABU KINGO ALIKUWA MTUMISHI WA TAZARA HADI KUSTAFU KWAKE LAKINI HADI SASA NI TAKRIBANI MIAKA ZAIDI YA SABA ANASUBIRI BILA YA MAFANIKIO

KATIKA UZAO WA BABU MZEE KINGO WA PWANI KISALAWE MZENGA ALIKUWA NA WATOTO WATANO WA KIUME NA WAWILI WA KIKE HADI SASA WAMEBAKI WAWILI WAKIUME NA KIKE WAWILI AKIWA NDIO WAMWISHO KUZALIWA NA AMEFARIKI KWA TATIZO LA UGONJWA WA MOYO LAKINI NIWAONAPO KAKA ZAKE NA DADA ZAKE HAWA NAFARIJIKA SANA


KULIA NI SHANGAZI YANGU MKUBWA NA DADA ZANGU TUKIONGEA MENGI, SHANGAZI AMEPATWA NA UGONJWA WA KUPOOZA UPANDE WA KUSHOTO SASA ANAENDELEA NA MATIBABU NA MAZOEZI MUNGU NI MWEMA ANGALAU SASA ANAUWEZO WA KUJITEGEMEA

UKAFIKA MCHANA ILIKUWA SIKU MBAYA KUKOSA UGALI WA MHOGO NIKAPOZA NJAA KWA UGALI SEMBE NA KISAMVU
KINGOTANZANIA
Post a Comment