Akizungumza na vyombo vya habari
mara baada ya kukagua mitambo ya kusindika gesi katika kisiwa hicho Profesa Muhongo amesema, uwekezaji uliofanywa na
serikali ya NORWAY ni wa kihistoria na kwamba umeipa changamoto serikali ya
Tanzania ambayo iko mbioni kuanza uzalishaji mkubwa wa gesi na Mafuta katika
mikoa ya Kusini.
Akijibu swali la mwandishi wa
habari kutoka gazeti la serikali la NORWAY Profesa MUHONGO amesema kutokana na
matumizi ya teknolojia ya kisasa ya kusindika gesi katika nchi zilizoendelea,
serikali ya Tanzania imeamua kuzitembelea baadhi ya nchi zenye teknolojia hiyo
ili kuhakikisha sera ya gesi inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni
inatekelezwa kulingana na matakwa ya wadau pamoja na mazingira ya eneo husika.
Muhongo amesema kupitia ziara
hiyo amejifunza mambo muhimu kupitia miundombinu ya kuzindika gesi nchini Norway
ilivyojegwa na kwamba uwekezaji wa gesi unahitaji technolojia ya hali ya juu
pamoja na rasilimali fedha mambo ambayo yamesaidia kubadili historia ya Norway
kupitiamitambo ya usindikaji wa gesi ambapo NORWAY Imetumia kiasi cha dola za
kimarekani bilioni 10 Kufanikisha mradi huo.
Halikadhalika Profesa Muhongo
amesema dhana ya ushirikishwaji wa wananchi katika utekelezaji wa miradi ya
umma halipaswi kupuuzwa na kwamba mradi wa gesi utakaoanza nchini Tanzania kwanza utatatua matatizo ya wazawa ikiwa ni
pamoja na kutumika katika kuzalisha nishati ambayo inahitajika kwa kiasi
kikubwa na baadaye kuuzwa nchi jirani.
Muhongo amesisitiza kuwa watanzania watanufauka na uwekezaji huu kwani
serikali inajipanga kuwasaidia wananchi ili waweze kunufaika na mradi mkubwa wa
gesi katika masuala ya elimu, afya, barabara, maji na kama jinsi jamii zilizopo karibu na makampuni
ya gesi na mafuta nchini Norway zinavyonufaika.
Kwa upande wake balozi wa Norway nchini
Tanzania Bibi Ingunn Klepsvik alisema
nchi yake iko tayari kubadilishana uzoefu na Tanzania na kuahidi kuwabega kwa
bega na Tanzania katika kuboresha miradi ya gesi ambayo ndiyo kwanza inaanza
nchini.
Ingunn amesema Norway ilianza
kuwekeza katika sekta ya gesi kwa kutegemea wataalamu toka Marekani ambapo
waliwawezesha kupata utaalamu katika masuala ya gesi mpaka pale walivyoweza
kuendesha mitambo wao wenyewe na kuwezesha kuinua kipato cha watu wa
Norway.
Kwa upande wake Meneja rasilimali
watu na mafunzo toka TPDC Flora Salakana amesesema uzoefu alioupata toka hammerfest
utasaidia katika kuboresha mipango ya serikali katika kuwaendeleza wataalamu wa
tanzania kushiriki kikamilifu katika miradi ya utafutaji, uzalishaji na
uendelezaji wa gesi asilia Tanzania.
Pia amesema Serikali ya Norway
kupitia kampuni ya Statoil itabadilishana uzoefu na wataalamu wa kitanzania
toka (TPDC) hivyo kuwawezesha kufanya mafunzo ya vitendo kwenye mitambo ya
kusafisha gesi asilia na kuwawezesha watanzania kujinoa kiutaalamu kwa njia
hiyo kupitia Norway.
Salakana amesema uhusiano huu ni
mwendelezo wa ushirikiano uliodumu kwa muda mrefu baina ya nchi hizi mbili na kwamba wataalamu wengi wa TPDC wamepata mafunzo yao
nchini Norway.
Mwishoni mwa miaka ya 1960 na
1970 Ugunduzi wa gesi asilia nchini Norway lakini iliwachukua miaka kadhaa
mpaka pale walipoanza kunufaika na uwekezaji huo miaka ya 2004 na mnamo mwaka
2007 Norway ilianza kujishughulisha na usindikaji wa gesi asilia iliyosaidia
katika kuingiza pesa nyingi za kigeni nchini Norway na
kuboresha maisha ya watu wake.
No comments:
Post a Comment