Monday, October 7, 2013

Vijana wakamatwa msituni Mtwara na CD zenye mafunzo ya al-Qaeda, al-Shabaab

zzzzzkamanda_mtwara_ca9c9.jpg
Na Abdallah Bakari, Mtwara 

POLISI mkoani Mtwara inawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kupata mafunzo ya kijeshi msituni kwa kutumia CDs za al-Shabaab.

Tukio hilo la aina yake limetokea katika mlima Makolionga wilaya ya Nanyumbu mkoani hapa ambapo pia CDs zenye mafunzo mbalimbali ya kijeshi 25 zimekamatwa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, Zelothe Stephen ameuambia "mtandao wa Kusini Leo" kuwa watuhumiwa hao
walikamatwa wiki moja iliyopita baada ya jeshi lake kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema: "CD hizo zilikuwa zinatoa mafunzo ya Al-Shabaab ya kuchinja watu, Mauaji wa Osama Bin Laden, Zindukeni Zanzibar, Kuandaa Majeshi, Mauaji wa Idd Amin na Mogadishu Sniper," alisema Stephen.


Alisema watuhumiwa wote ni wakazi wa wilaya ya Nanyumbu mkoani hapa na kwamba walikuwa wakiongoza na Mohamed Makande 39, mkazi wa kijiji cha Sengenya ambaye pia anashikiliwa na jeshi hilo.
Aliwataja wengine waliokamatwa kuwani Hassan Omary (39) mkazi wa kijiji cha Nanyulu, Rashid Ismail (27). Abdallah Y. Hamisi (32), Salum Wadi (38), Fadhili Rajabu (20), Abbas Muhidini (32), Ismail Chande (18), Said Mawazo, Issa Abeid (21), na Ramadhani Issa (26) wote wakazi wa kijiji cha Likokona.

Kuhusu vitu watuhumiwa walivyokamatwa navyo, Kamanda Zelothe alisema, "Tumekamata mapanga mawili, Deki ya DVD, Solar, Visu, Tochi, Betri, Simu za kiganjani 5, Vyombo mbalimbali vya kulia chakula, Baiskeli tatu, Vitabu mbalimbali wa dini ya Kiislam, Unga wa mahindi kilo 50, Mahidi kilo 150 na virago vya kulalia. Vingine ni mfuko wa kijani unaosadikiwa ni wa kijeshi wenye nembo ya nanga ya meli yenye mistari kulia na kushoto na nyoka katikati."

Alisema jeshi lake licha ya kuwafikisha watuhumiwa mahakamani, linaendelea na uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na Polisi Makao Makuu kwa lengo la kufanikisha kuunasa mtandao mzima.
Source: http://www.wavuti.com

No comments: