Thursday, November 14, 2013

Barabara ya Lami kutoka Sumbawanga kwenda Jijini Mbeya Sehemu kubwa ya Barabara hiyo kwa sasa imeshakalika

Gari anayoitumia Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa Ndugu Philip Mangula ikitembea katika barabara ya Lami kutoka Sumbawanga kwenda Jijini Mbeya. 
 
Sehemu kubwa ya Barabara hiyo kwa sasa imeshakalika hususani miradi miwili ya Tunduma – Ikana na Ikana – Laela, mradi mmoja wa Laela-Sumbawanga unaojengwa na Mkandarasi Aasleaff Bam International ambao ulikua unasusua sasa unaendelea kwa kiwango cha kuridhisha. Maendeleo haya ya barabara na mengine mengi aliyoyaona yalikua kivutio kikubwa kwa Mhe. Mangula ambae alitoa ushuhuda kwamba tangu afike Mkoani Rukwa mara ya mwisho mwaka 2003 na sasa hali ni tofauti kabisa na kwamba kwa kipindi hicho cha Miaka 10 ameioana Rukwa Mpya.
 
KINGOTANZANIA
Post a Comment