Tuesday, November 26, 2013

Chadema ' Civil War' Imepamba Moto...!

MOTOOO_3daf8.jpg
Ndugu zangu,

Chadema ' Civil War' imepamba moto. Media imeripoti kuwa leo Chadema Makao Makuu watajibu mapigo. Bado moshi wa makombora ya Zitto haujatua. Ni juzi Zitto alitoka kwenye handaki na kajibu mapigo. Na kama ilivyotarajiwa, Chadema nao wametoka kwenye handaki. Nao wamejipanga kufanya mashambulizi leo. Naam, siasa ni burudani pia. Kuna wengi watasubiri kwa hamu.


Bila shaka, Chadema watakwenda kuyaonyesha mashimo kwenye utetezi wa Zitto juzi. Watazama sana kwenye Katiba yao na kuonyesha walivyo makini katika kuifuata.
Ni nini kinachoendelea ?

Tafsiri yangu kiini ni mgogoro wa uongozi ndani ya Chadema. Ni mgogoro wenye kuiweka Chadema kwenye hatari ya kugawanyika. Na kama nilivyobainisha juzi, unahusu uongozi na mamlaka na hususan kuelekea 2015 na mbele zaidi.

Kuna mahali wahusika, kama watataka kupata - win-win situation, itawabidi wakae meza moja na kukubaliana. Lakini, inavyoonekana sasa, hakuna mwenye haja ya matokeo ya suluhu. Ni lazima mmoja apigwe. Na kama nilivyobainisha juzi, kuwa atakayeshindwa, basi, itakuwa ni mwanzo wa mwisho wake wa kuwepo katika hali aliyo nayo sasa.

Na nilisema, kuwa ' Vita' hii itapiganwa kwanza kwenye media. Na baada ya hapo itahamia kwenye mikutano ya hadhara. Ndio, na tuisubiri ' Kamukunji' .

Maggid Mjengwa

Post a Comment