Monday, November 25, 2013

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AKIWA WILAYANI RUNGWE

1
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto akipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Ndugu Bw. Crispin Meela katika mji wa Ushirika wilayani Rungwe mara baada ya kuwasili wilayani huo, akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mbeya ambayo aliianza jana wilayani Kyela akitokea Mbamba Bay wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma , Kinana ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa , Kinana ameanza kazi katika wilaya ya Rungwe kwa kufanya mkutano wa ndani ambapo atapokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na uhai wa chama wilayani Rungwe 2Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Rungwe Mashariki Mh. David Mwakyusa mara baada ya kuwasili katika mji wa Ushirika Wilayani Rungwe ambapo ndipo alipopokelewa leo
3Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia jambo na Richard Kasesela mmoja wa wana CCM waliofika kwenye mapokezi hayo. 5Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akisalimiana na Richard Kasesela katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Nd. Crispin Meela. 6Baadhi ya viongozi wa CCM wilayani Rungwe wakiwa katika mkutano wa ndani ambao Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana atapokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM unaofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri mjini Tukuyu. 7Baadhi ya wajumbe wakimpokea Ndugu Abdulrahman Kinana tayari kwa kikao hicho cha ndani. 8Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya na Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki Mh Godfrey Zambi ,Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wakisaini vitabu vya wageni mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mkutano mjini Tukuyu.
Katibu wa NEC Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara Kandete Wilayani Rungwe.

Katibu wa NEC Uhusiano wa Kimataifa Dr. Asha Rose Migiro akitoa shukrani kwa wananchi wa wilaya ya Rungwe kwa kugalagal chini baada ya upewa zawadi na akina mama wa Halmashauri ya Busokelo.

Viongozi wa CCM WILAYA YA Rungwe wakisikiliza hotuba za viongozi wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu, Abdulrahman Kinana katika kata ya Kandete wilayani Rungwe.

MSAFARA NDANI YA HALMASHAURI YA BUSOKELO

Post a Comment