Mkurugenzi
Mkuu wa Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akielezea kwa waandishi
wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam mapema hii leo juu ya
mikakati ya kuinua utalii hifadhi za kusini na magharibi kwa kutenga
maeneo 34 ya uwekezaji, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari
(MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa.
Baadhi ya
waandish wa Habari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi
za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi wakati akielezea mikakati ya kuinua
utalii hifadhi za kusini na magharibi kwa kutenga maeneo 34 ya
uwekezaji.
Na Jovina Bujulu-Maelezo
Tanzania
inaongoza kwa kuwa na vivutio bora vya utalii barani Afrika,utafiti
uliondeshwa na mtandao wa safaribookings.com wa nchini uholanzi
umebainisha.
Taarifa
iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA)
bw.Allan Kijazi alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar
es salam.
Bw.
Kijazi alibainisha kuwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ilikuwa ya kwanza
kati ya vivutio 50 bora Barani Afrika ambapo vivutio 10 kati ya hivyo
viko Tanzania.
Alivitaja
vivutio vilivyoongoza kuwa ni Ruaha,Mahale,Gombe,Katavi,Tarangire,ziwa
Manyara na Arusha,Vingine ni Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na pori la
akiba la selous.
Akizungumzia
faida za kuwa na vivutio bora ,ndugu kijazi alisema kwamba wingi na
ubora wa vivutio hivyo umetoa fursa ya pekee kwa wawekezaji kuwekeza
kwenye maeneo mbalimbali katika hifadhi hizo hivyo kuongeza pato la
Taifa.
Aidha
ndugu Kijazi aliongeza kwamba TANAPA imetenga maeneo 34 kwa ajili ya
kupanua wigo wa huduma za malazi katika hifadhi za Taifa ambapo
kipaumbele ni kwenye hifadhi za kusini na magharibi ya nchi ambazo zina
uhaba wa malazi na hivyo kusababisha idadi ndogo ya watalii kutembelea
maeneo hayo.
Bw.
Kijazi alimaliazia kwa kusema kwamba wanategemea kuongeza idadi ya
watalii kutokana na maboresho hayo na hivyo kukuza pato la Taifa
kutokana na sekta ya utalii.
No comments:
Post a Comment