Tuesday, November 12, 2013

Waliomuua mwenyekiti wa Halmashauri ya Rungwe John Mwankenja wawili wahukumiwa kunyongwa wengine kifungo miaka saba habari kamili itawajia

MMOJA WA WAUUAJI WA JOHN MWANKENJA AMBAYE ALUKUWA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA RUNGWE BAADA YA KUOMEWA HUKUMU YA KUNYONGWA HADI KUFA NA WENGINE HUKUMU YA MIAKA SABA KUMILIKI SIRAHA ILIYOTUMIKA KATIKA MAUAJI YA MWANKENJA

KATIKATI NI ALIYEKUWA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA RUNGWE JOHN MWANKENJA KABLA YA KIFO AKIONGOZA KIKAO CHA MADIWANI WILAYA YA RUNGWE
SEHEMU YA MAUAJI YA MAREHEMU JOHN MWANKENJA AMBAYE ALIKUWA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA RUNGWE

VIPANDE VYA FUVU LA KICHWA NA UBONGO PAMOJA NA DAMU BAADA YA MAUAJI YA KUTISHA YA MAREHEM JOHN MWANKENJA

GALI ALIMOKUWEMO MAREHEM JOHN MWANKENJA BAADA YA KUTOKA SAFARI YA KUMUONA MKEWE KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA AKAPAKI GALI HAPA NYUMBANI KWAKE HUKU WATOTO WAKE WAKISHUSHA MIZINGO NYUMA YA GALI NDIPO WAUAJI WAKATOKEA  NA KUANZA KUMSHAMBULIA KWA RISASI NA KUSABABISHA KIFO HAPOHAPO KWENYE KITI KABLA HAJASHUKA KWENYE GALI
MKE WA MAREHEMU JOHN MWANKENJA SIKU YA MAZIKO YA MUMEWE AMBAYE NI MTUMISHI WA SERIKALI HALMASHAURI YA RUNGWE AKIWA NDIO MKUU WA KITENGO CHA TASAFU HAPO AKIWASILI KUTOKA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA AMBAKO ALILAZWA  AKISUBIRI UPASUAJI
PROF MWANDOSYA MBUNGE WA RUNGWE MAGHARIBI AKIONGEA KWENYE MAZIKO YA JOHN MWANKEJA AKIONGEA KWA MAJONZI MAZITO KUHUSIANA NA KIFO CHA MWANKENJA MWANDOSYA ALILAANI KIFO HICHO NA KUITAKA JAMII NA JESHI LA PILISI KUHAKIKISHA WALIOHUSIKA WANAKAMATWA NA KUFIKISHWA KATIKA CHOMBO CHA DORA HIVYO LEO TAREHE 12.11.2013 MAHAKAMA YA WILAYA IKIONGOZWA NA JAJI BAADA YA KUENDESHWA KWA KESI KWA MUDA SASA HUKUMU IMETOKA NA KUWA WATU WAWILI KIFUNGO CHA MAISHA NA WENGINE MIAKA SABA KWA KUMILIKI SIRAHA ILIYOTUMIKA KATIKA MAUAJI. 

WATUHUMIWA WANNE WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO LA MAUAJI YA MAREHEMU JOHN MWANKENJA WAPATIKANA NA HATIA MAHAKAMANI

MAJAMBAZI 8
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA. 

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 13. 11. 2013. 
             
WILAYA YA RUNGWE – WATUHUMIWA WANNE WALIOHUSIKA NA
TUKIO LA MAUAJI YA MAREHEMU JOHN
AFWILILE MWANKENJA 

§  MNAMO KATI YA  TAREHE 12.11.2013 KATIKA KIKAO CHA MAHAKAMA KUU KANDA YA  MBEYA   KILICHOFANYIKA TUKUYU WILAYA YA  RUNGWE  MKOA WA  MBEYA, WATUHUMIWA WATATU 1.AKIMU S/O MSELEM MWAKALINGA , 2. DAUDI S/O JUSTI MWASIPASA, 3. OBETE S/O MWANYINGILI ANGANISHE MASUNGO NA 4. KELVIN S/O MAURUS MYOVELA WALIPATIKANA NA HATIA KUFUATIA KUHUSIKA NA TUKIO LA MAUAJI YA  ALIYEKUWA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA  WILAYA YA  RUNGWE MAREHEMU JOHN AFWILILE MWANKENJA.

§  KATIKA  HUKUMU ILIYOSOMWA NA MHE JAJI S.VJ. KARUA,   WATUHUMIWA  AKIMU S/O MSELEM MWAKALINGA NA DAUDI S/O JUSTI MWASIPASA WALIHUKUMIWA  HUKUMU YA  KIFO [KUNYONGWA]  NA WATUHUMIWA OBETE S/O MWANYINGILI ANGANISHE MASUNGO NA KELVIN S/O MAURUS MYOVELA WALIHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA SABA [07] KWA KUSAIDIA KUTENDEKA KWA KOSA. 

§  AWALI MNAMO TAREHE 19.05.2011 MAJIRA YA  SAA 20:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA KIWIRA, KATA YA  KIWIRA ,WILAYA YA  RUNGWE, MKOA WA MBEYA, MAREHEMU JOHN S/O AFWILILE MWANKENJA, MIAKA 50, KYUSA,  ALIYEKUWA M/KITI WA HALMASHAURI YA  WILAYA YA  RUNGWE,  DIWANI WA KATA YA  KIWIRA NA  PIA MWENYEKITI WA CCM WILAYA HIYO AKIWA ANATOKEA MBEYA MJINI NA GARI T.127 ACZ AINA YA  NISSAN DOUBLE CABIN ALIPOFIKA ENEO LA NYUMBANI KWAKE ALIPIGWA  RISASI NNE KICHWANI NA KUFARIKI DUNIA PAPO HAPO. 
§  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHANA NA UOVU/UHALIFU WA AINA YOYOTE ILE ILI KUJENGA JAMII NA NCHI ILIYOBORA NA YENYE MAENDELEO. 
 
            WILAYA YA  RUNGWE  – MTUHUMIWA MMOJA APATIKANA NA HATIA KWA KOSA LA
KUBAKA NA KUUA MTOTO MDOGO.
§  MNAMO TAREHE 12.11.2013 HUKO  KATIKA KIKAO CHA MAHAKAMA KUU KANDA YA  MBEYA KILICHOFANYIKA TUKUYU WILAYA YA  RUNGWE  MKOA WA  MBEYA, MTUHUMIWA BARAKA  S/O JAILO MWANDEMBO,MIAKA 34,KYUSA, MFANYABIASHARA, MKAZI WA BULYAGA – TUKUYU  ALIPATIKANA NA HATIA KUFUATIA KUHUSIKA NA TUKIO LA MAUAJI YA  MTOTO MDOGO MWENYE MIAKA MITANO.
§  AWALI MNAMO TAREHE 21.01.2010 MAJIRA YA SAA 17:00HRS MTUHUMIWA ALIONEKANA AKIONGEA NA MTOTO HUYO NA KISHA MTOTO KUPOTEA KATIKA MAZINGIRA YA  KUTATANISHA. WANANCHI KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI WAKIWA KATIKA MSAKO WA KUMTAFUTA MTOTO HUYO TAREHE 22.01.2012 MAJIRA YA SAA 00:30HRS MAREHEMU ALIKUTWA KICHAKANI AKIWA HANA JERAHA UMBALI WA KILOMITA 1 KUTOKA NYUMBANI KWAO AKIWA AMEBAKWA  KISHA KUUAWA. 
§  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA MARA MOJA UOVU/UHALIFU WA AINA YOYOTE ILE ILI KUJENGA JAMII ILIYOBORA NA YENYE MAENDELEO. 
 [DIWANI ATHUMANI   - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA. 

Post a Comment