Kamanda
wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna (CP), Suleiman
Kova (kulia), akionesha mapanga kwa waandishi wa habari na mbele ya
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto), Dar es Salaam
jana, yaliyotumika kumshambulia Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Mabadiliko ya
Katiba Mpya, Dk.Sengondo Mvungi wakati akitoa taarifa ya kukamatwa kwa
watuhumiwa tisa walioshiriki katika tukio hilo.
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na waandishi
wa habari kuhusiana na tukio la kuvamiwa na kushambuliwa Dk Sengondo
Mvungi, Mjumbe wa Tume ya Katiba. Waziri Nchimbi alisema upepelezi wa
tukio hilo umefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 80 ambapo tayari watuhumiwa
tisa wamekamatwa wakiwa na mapanga na simu moja ya mkononi, watuhumiwa
hao walitajwa majina yao katika mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Hata hivyo,
Waziri Nchimbi aliwaomba wananchi na waandishi wa habari wawe na subira
wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi kwa ajili ya kuwakamata
watuhumiwa wengine. Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame
Silima. Kulia ni Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam,
Suleiman Kova.
Kamishna
wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova akiwaonyesha
waandishi wa habari mapanga waliyoyakamata wakati wa msako mkali wa
kuwasaka watuhumiwa waliomvamia na kumshambulia Dk Sengondo Mvungi
Mjumbe wa Tume ya Katiba. Katika msakao huo watuhumiwa tisa walikamatwa
wakiwa na mapanga na simu moja ya mkononi. Katikati (waliokaa meza kuu)
ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi. Kushoto ni
Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Hata hivyo, Waziri
Nchimbi aliwaomba wananchi na waandishi wa habari wawe na subira wakati
Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi kwa ajili ya kuwakamata
watuhumiwa wengine. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment