Monday, December 9, 2013

Dr Jakaya Kikwete Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania awaongoza watanzania katika Maadhimisho ya miaka 52 ya Tanganyika...

jkuhuru_6fd0f.jpg
Raisi Jakaya M. Kikwete akiwasili kwenye uwanja wa Taifa wa Uhuru ili kuwaongoza watanzania katika maadhimisho ya miaka 52 ya uhuru wa Tanganyika. Tanganyika ilipata uhuru mwaka 1961 tarehe 9 Desemba. Watanzania wengi wamekusanyika kwenye uwanja wa Uhuru ili kuweza kuungana na watanzania wengine katika maadhimisho haya.
Picha na 1 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi alipokua akiwasili uwanja wa Uhuru wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru leo jijini Dar es salaam.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange.
Picha na 2 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akipokea salam ya Rais na kupigiwa mizinga 21 kutoka kwa gwaride la vikosi vya majeshi ya Ulinzi ya Tanzania leo uwanja wa Uhuru mara baada ya kuwasili.
Picha na 3  
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya majeshi ya Ulinzi na usalama leo uwanja wa Uhuru wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru.Picha na 4  
Sehemu ya askari wa vikosi vya ulinzi na usalama wakiwa wamesimama kwa ukakamavu wakati kabla ya kamanda wa gwaride kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kukagua gwaride hilo leo jijini Dar es salaam.Picha na 5  
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete  akiwasili jukwaa kuu la Uwanja wa Uhuru wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru Picha na 6  
 Gwaride likipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa mwendo wa haraka.Picha na 7  
Rais Jakaya Kikwete na Amiri Jeshi Mkuu akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange wakati gwaride la vikosi vya Ulinzi na Usalama likipita mbele ya jukwaa kuu  la uwanja wa Uhuru kwa mwendo wa haraka.Picha na 8 
Baadhi ya Maofisa wa jeshi wakipiga saluti wakati wimbo wa Taifa ukiimbwa wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru leo jijini Dar es salaam.
Picha na 9 Wananchi wa mkoa wa Dar es salaam waliojitokeza kuhudhuria maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru uwanja wa Uhuru leo jijini Dar es salaam.Picha na 10 
Vijana wa halaiki kutoka Tanzania Bara na Visiwani wakitamka kauli mbiu ya maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara leo jijini Dar es salaam ambayo ni “ Vijana ni Nguzo ya Rasilimali Watu,Tuwaamini, Tuwawezeshe na Tuwatumie kwa Manufaa ta Taifa Letu”Picha na 11 
Vijana wa halaiki wakiendelea kuwasilisha jumbe mbalimbali kama inavyoonekana mfano wa mnyama aina ya simba kuashiria utalii katika hifadhi  za wanyama za Tanzania.
Picha na 12  
Vijana wa halaiki wakionyesha ukakamavu kwa kuonyesha sanaa ya sarakasi Picha na 14  
Ujumbe ukiwasilishwa kwa njia ya picha kuhusu viongozi wapigania Uhuru wa Tanzania Bara, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.Picha na 15 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akitoa hatuba fupi kwa watanzania wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Hatuba yake licha ya kujaa maneno ya kumkumbuka rais wa kwanza wa Afrika ya Kusini  Mzee Nelson Rolihlahla Mandela Madiba  aliyeaga dunia juzi nchini Afrika ya Kusini imesisitiza Upendo, Amani, Mshikamano miongoni mwa  watanzania na kukemea tabia ya baadhi ya viongozi kulipiza kisasi pindi waingiapo madarakani.Picha na 16 
 Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein (kushoto), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) na Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange wakisoma Jarida la Nchi Yetu linalochapishwa na Idara ya Habari (MAELEZO) leo katika uwanja wa Uhuru wakati wa Maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru.Picha na 17 
Raia wa kigeni waliohudhuria sherehe za miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara wakisoma Jarida la Nchi Yetu linalochapishwa na Idara ya Habari MAELEZOPicha na 18  
Rais Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange alipokua akisoma Jarida la Nchi Yetu linalochapishwa na Idara ya Habari Picha na 19Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendelo Freeman Mbowe akiwa miongoni mwa viongozi wa vyama vya siasa waliohudhuria maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru.

 .....................................

Hakuna mahali pa kukanyaga’ msibani kwa Mandela

s b0103
Makazi ya Rais wa Kwanza mzalendo wa Afrika Kusini yaliyopo katika Mtaa wa Laa namba 12, Houghton ambako ndiko alikokuwa hadi alipokutwa na mauti, ni kama hapaingiliki kutokana na wingi wa watu, magari na vyombo vya habari kutoka sehemu mbalimbali duniani ambavyo vimeweka kambi katika eneo hilo, usiku na mchana kufuatilia safari ya mwisho ya kiongozi huyo.


Anga la mtaa huo na sehemu za jirani, limehanikizwa na sauti nyingi za nyimbo zikiongozwa na Wimbo wa Taifa wa Afrika Kusini 'Nkosi Sikeleli Afrika' (Mungu Ibariki Afrika), ukifuatiwa kwa zamu na nyimbo za kidini na zile za asili ambazo zinasifu ushujaa wa Mandela.

Katika lango la kuingia kwenye makazi hayo ya Mandela, kuna maombolezo ya aina yake kwani yameambatana na kitu ambacho kwa macho kinaonekana kama shamrashamra kwa nyimbo za sifa na kufurahia kile Waafrika Kusini wanachokiita kazi nzuri ya kutukuka ya Mandela aliyoifanya katika umri wa miaka 95 ya uhai wake.

Mwandishi wetui alitembelea makazi hayo ya Mandela jana na kushuhudia umati mkubwa wa watu wakifika nje ya nyumba yake kwa ajili ya kuomboleza; wakiweka mashada ya maua, mishumaa na kadi zenye ujumbe wa pole kwa familia yake.
Miongoni mwa waliokuwapo katika eneo hilo ni Mtanzania, Christer Mwageni na watoto wake; Sabina na Faraja.

Mwageni alisema: "Kwa jinsi hali ilivyo, huwezi kukwepa kuwa mwombolezaji, mimi na wanangu tulikuja hapa kutembea tu kwa siku tatu hivi lakini tumejikuta tukishiriki msiba na hata kama tungekuwa hatutaki kushiriki, uhalisia unatulazimisha".
"Kweli tuna mengi ya kujifunza, inaonekana msiba huu wa Mzee Mandela umewaunganisha zaidi Waafrika Kusini, maana wote bila kujali rangi wala kingine chochote, wanaonekana kuomboleza kwa dhati kutoka mioyoni kabisa."
Katika eneo hilo la Houghton, ulinzi umeimarishwa na polisi wako kila kona na wamekuwa wakiwaelekeza waombolezaji na watu wengine njia sahihi za kufuata hadi kuyafikia makazi ya Mzee Mandela kutoka na barabara nyingi za kuingia katika eneo kufungwa na nyingine kugeuzwa maegesho ya magari ya waombolezaji.

Kwa ujumla, pilikapilika ni nyingi, lakini katika lango kuu la kuingia makazi ya Mandela, ulinzi ni mkubwa na hakuna anayeruhusiwa kulikaribia isipokuwa wanafamilia, vingozi wa Serikali na watu wengine wenye shughuli maalumu.Soweto, Mandela Square
Hali kama hiyo ipo katika makazi yake ya zamani Mtaa wa Vilakazi Na: 8115, Orlando Magharibi, Soweto ambako kuna pilikapilika nyingi zinazoyahusisha makundi ya watu kutoka ndani na nje ya Afrika Kusini.Mandela aliishi katika Mtaa wa Vilakazi kabla ya kukamatwa na kuwekwa kizuizini na alirejea katika nyumba hiyo miaka 27 baadaye alipoachiwa huru na kuishi humo kwa siku kumi na moja kabla ya kuhamia katika nyumba ya aliyekuwa mkewe, Winnie Mandela katika eneo hilohilo la Soweto.
Kama ilivyo Houngton, katika eneo hilo pia ulinzi umeimarishwa na baadhi ya njia zimefungwa kutokana na wingi wa watu na magari. Vyombo vya habari kutoka kila pembe ya dunia navyo vipo vikiendelea kufuatilia maombolezo hayo.

Katika nyumba ya Soweto ambayo sasa ni makumbusho ya Mzee Mandela, idadi kubwa ya watu wanafurika kujifunza historia ya kiongozi huyo na nje vipo vikundi vinavyoimba nyimbo za maombolezo na kumsifu Mandela kwa ushujaa wake.
Eneo la tatu ni Mandela Square lililopo katika Jiji la Sandton, Johannesburg ambako kuna sanamu kubwa ya kiongozi huyo yenye urefu wa mita sita kwenda juu, likimwonyesha katika hali ya kucheza muziki. Iliwekwa katika eneo hilo, Machi 31, 2004.

Katika eneo hilo, pia ulinzi umeimarishwa na askari wanalazimika kusimamia jinsi watu wanaovyoingia na kutoka. Watu wamekuwa wakisimama katika msitari mrefu kupata fursa ya kupiga picha katika sanamu hiyo yenye uzito wa tani mbili na nusu (kilo 2,500).

Pembezoni mwa sanamu hiyo, kama ilivyo Houghton na Malakazi, limetengwa eneo maalumu kwa ajili ya watu wanaoomboleza kuweka maua, nembo, nyaraka na mishumaa.

Maombolezo ya kifo cha Mandela yanaingia katika siku ya nne leo na yataendelea hadi Jumapili ijayo ya Desemba 15 wakati kiongozi huyo atakapozikwa kijijini kwake Qunu, Mthatha Mkoa wa Eastern Cape

No comments: