Monday, December 9, 2013

HELIKOPTA YATUA UWANJANI BRAZIL KUBEBA MAJERUHI

article-2520380-19F6D4A900000578-407_634x374_c121a.jpg
HELIKOPTA ilitu uwanjani kubeba majeruhi baada ya kutokea vurugu katika mechi ya soka Brazil jukwaani baina ya mashabiki.

Mchezo kati Atletico PR na Vasco da Gama, ulisimamishwa Jumapili baada ya mashabiki kuanza kupigana wenyewe kwa wenyewe. Mashabiki waliokuwa wanapigana ilibidi watenganishwe na Polisi wa kutuliza ghasia kwa kuwafyatulia mabomu.
Mchezo huo ukaanza tena baada ya saa moja na dakika 10 za kusimama kupisha vurumai.
Tukio hili ni baya kwa Brazil, na litaifanya nchi hiyo ijipange kwa matukio ya aina hiyo wakati wa Fainali za Kombe la Dunia.
article-2520380-19F6FFFE00000578-356_634x357_f64e4.jpg
Mashabiki waliojeruhiwa wakibebwa kupelekwa kwenye helikopta
article-2520380-19F6F38700000578-197_634x425_e34cb.jpg
Mashabiki wa Atletico wakimtimba mateke shabiki wa Vasco da Gama

No comments: