Sunday, December 8, 2013

IGP MWEMA ATEUA MAKAMANDA WA MWANZA, MBEYA NA SIMIYU

mwema
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA


Aidha, Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mara Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Jafary Ibrahim amehamishiwa Kanda Maalum ya  Dar es Salaam  kuwa Mkuu wa Upelelezi na nafasi yake inachukuliwa na Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Rogathe Mlasani kutoka Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam.

Wengine ni Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) David Mnyambuga kutoka Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam anaenda kuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Tabora, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Martin Otieno kutoka Kanda Maalum ya Dar es salaam  amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi kuwa Mkuu wa kitengo cha Teknohama na Mrakibu wa Polisi (SP) Gidion  Msuya ambaye alikuwa Kaimu Mkuu wa Upelelezi  wa mkoa wa Tarime Rorya amehamishiwa  Tunduru kuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD).

Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

.................................................

SOMA ZAID.....

KINANA AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI PORINI, AOMBOLEZA KIFO CHA NELSON MANDELA

12
1a 1b 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusimama njiani akitokea wilayani Makete akielekea  wilayani Wanging”ombe, katika ziara yake maalum ya Mkoa wa Njombe  kuhusu Chama cha Mapinduzi kilivyopokea kifo cha mpigania uhuru wa Afrika Kusini na mtu aliyeheshimiwa sana duniani Mzee Nelson Mandela kama alivyojulikana kama “Madiba” aliyefariki dunia  usiku wa kuamkia leo ijumaa tarehe 6, Kinana amesema CCM inatambua jinsi Nelson Mandela alivyoipigania nchi yake na Afrika kwa ujumla, kuikomboa mikononi mwa ubaguzi wa rangi na kuiweka huru, Ameongeza kwamba CCM na wanachama wake pamoja na watanzania wote watakumbuka mambo mema yote aliyoifanyia nchi yake na Afrika kwa ujumla na kuyaenzi kwa vitendo. 2a 
Katibu Mkuu wa Cchama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza mara baada ya kukagua shule ya sekondari ya Makete Girls iliyopo katika kijiji cha Mtweve wilayani Makete leo akiwa njiani kwenda Wilayani Wanging”ombe, kutoka kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi, Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa na wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephin Matiro. Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephin Matiro akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kukagua sekondari ya Makete Girls katika kijiji cha Mtweve akiwa njiani kwenda Wanging”ombe mkoani Njombe, Kutoka kulia ni Toto Timoth ambaye ametoa tani tano ya mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo,Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi na  Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa 5  
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika kijiji cha Usuka kilipo kituo cha Mafunzo ya zana za kilimo kwa wakulima wilayani Wanging’ombe ambapo Katibu mkuu wa CCM alitembelea vijana walioamua kujiunga pamoja na kuendesha kilimo .  14 
 IMG_2522 
Juhudi za kunasua zikiendelea. 22 

No comments: