Wednesday, December 11, 2013

Mandela aivuta dunia kuhamia Afrika Kusini.............

mandelaclip_5a08c.jpg
Na Neville meena, Mwananchi

http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2013/12/ma2.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa na Rais Mstaafu wa Marekani Mhe George W. Bush na Mkewe Laura Bush wakiwa jukwaa la viongozi na watu mashuhuri baada ya Kuadhimisha Kumbukumbu ya Kifo cha aliyekuwa kiongozi mashuhuri wa Afrika Kusini na duniani, Mheshimiwa Nelson R Mandela leo Desemba 10, 2013 katika uwanja wa FNB jijini Johannesburg.PICHA NA IKULU


ma4

DSC04708 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa na Rais wa kwanza wa Arika ya Kusini Mzee Nelson Mandela enzi za uhai wake wakati walimpomtembelea kwenye ofisi ya Taasisi yake jijini Johanesburg tarehe 12 Julai mwaka 2006. Rais Kikwete jana aliondoka kwwneda Afrika ya kusini kuungana na viongozi wengine kwenye ibada ya mazishi ya mzee Mandela

Johannesburg. Viongozi zaidi ya sabini wakiwamo wakuu wa nchi na Serikali wanatarajiwa kushiriki hatua mbalimbali za safari ya mwisho ya Mzee Mandela aliyefariki Alhamisi ya Desemba tano usiku.
Anatarajiwa kuzikwa Jumapili ijayo, Desemba 15, 2013 katika Kijiji cha Qunu alikokulia, mazishi ambayo yanatarajiwa kuwavuta maelfu ya watu kutoka kona mbalimbali za dunia.

Hata hivyo hadi jana maofisa wa Serikali ya Afrika Kusini walisema walikuwa bado hawajapata orodha kamili ya viongozi wote watakaohudhuria, l pia wakashindwa kusema iwapo Rais Obama atakwenda Qunu au atashiriki katika hatua nyingine za awali za msiba huo kabla ya mazishi ya Jumapili.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Jay Carney alinukuliwa akithibitisha kwamba Obama na mkewe Michele watashiriki katika msiba huo lakini hakuwa tayari kueleza suala hilo kwa undani. Habari zaidi zilizopatikana jana mjini Johanesburg zinasema Rais wa Brazil, Dilma Rousseff atakuwa miongoni mwa wageni mashuhuri watakaoshiriki.

Balozi wa Marekani nchini Afrika Kusini, anasema kuwa: "Rais Obama, amethibitisha kushiriki mazishi ya Madiba" (akirejea) jina maarufu la Mzee Mandela, taarifa ambayo ilitiliwa na nguvu na habari zilizoinukuu Ikulu ya Washington ikithibitisha ujio wa kiongozi huyo pamoja na watanguliza wake; George W. Bush na Bill Clinton.

Vyombo mbalimbali vya habari vilinukuu taarifa ya Ikulu ya Marekani ikisema: "Rais Obama na mkewe watakwenda Afrika Kusini wiki ijayo kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kwa ajili ya kumbukumbu ya Nelson Mandela na watashiriki katika tukio hilo la kukumbukwa."
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma alitangaza ratiba ya maombolezo ya shujaa huyo aliyeongoza vita dhidi ya sera za ubaguzi wa rangi zilizokuwa zikitekelezwa na Makaburu na jana ilikuwa ni siku ya maombi ya kitaifa kwa ajili ya Mzee Mandela.

Leo Jumanne kutakuwa na tukio la kitaifa katika Uwanja wa Michezo wa FNB, Johannesburg ambako ni sehemu ya hitimisho ya safari ya Mandela huku watu zaidi ya 80,000 wakitarajiwa kuhudhuria na kati ya kesho Jumatano na Ijumaa, mwili wa Mandela utakuwa katika Majengo la Umoja (Union Buildings) Pretoria ambako utaangwa kwa siku tatu mfululizo.

Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Afrika KusiniNeo Momodu aliwaambia waandishi wa habari jijini Johannesburg kuwa watuwa Pretoria watakuwa na nafasi ya kushuhudia mwili wa Mandela ukisafirishwa kutoka chumba cha kuhifadhia maiti kwenda Jengo la Umoja kila asubuhi kwa siku tatu mfululizo.

Momudu anasema mitaa ambayo mwili huo utakuwa ukipitishwa itatangazwa ili kuwezesha wakazi wake na wananchi wengine kupata fursa ya kujipanga pembezoni mwake kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kwa kiongozi huyo.

"Njia ambazo mwili wa marehemu utakuwa ukipitishwa kila asubuhi kutoka chumba cha kuhifadhia kwa ajili ya kupelekwa kupewa heshima za mwisho, zitatangazwa na tutawaomba wananchi kujipanga pembezoni mwa njia hizo wakati mwili huo ukipita katika mitaa hiyo ya Pretoria," anasema.

Hata hivyo, Momodu anasema utaratibu wa kutoa heshima za mwisho utaratibiwa na kuna uwezekano mkubwa kwamba si kila mtu atakayeweza kuingia katika eneo hilo na kwamba kila mmoja atakayeingia lazima awe na kitambulisho maalumu

Anasema kutakuwa na eneo maalumu la kusubiri kuingia kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho na kwamba watakafanikiwa kupata ruhusa ya kwenda kuaga, watakuwa wakipakiwa kwenye mabasi maalumu yaliyoandaliwa kwa ajili ya kazi hiyo na watarejeshwa na mabasi hayo.
Jumamosi, Desemba 14, mwili wa Mandela utasafirishwa kwenda Qunu ambako Jumapili Desemba 15, utazikwa rasmi.

No comments: