Sunday, January 5, 2014

MAMA MGIMWA ACHANGANYIKIWA NA KIFO CHA MWANAE WA KWANZA NA KUSEMA"Mimi sikuwahi kufahamu wala kupata taarifa kama mtoto wangu anaumwa na amepelekwa kutibiwa Afrika ya kusini sasa naletewa maiti"


DSC 1018 9e3e7
Kaburi ambamo utazikwa mwili wa marehemu William Mgimwa kesho Jumatatu.

DSC 1026 e7b62
Mama yake marehemu Mgimwa, Bi Consolata Mgovanu (katikati).DSC 1033 f4ab3
Na Berdina Majinge, Iringa

MAMA mzazi wa aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Jimbo la Kalenga mkoani Iringa, William Mgimwa, amesema ameshtushwa na kifo cha mwanawe huyo wa kwanza (MNYAMA)
na kusema hakujua hata ugonjwa wake.

Consolata Mgovano, ambaye ni mama mzazi wa marehemu, aliliambia amesema kuwa amepokea taarifa ya kifo cha mwanae kwa masikitiko makubwa kutoka na kutokupata taarifa kuwa mwanae alikuwa anaumwa na amepelekwa afrika kusini kutibiwa na hatimaye kufariki dunia wakati anaendelea na matibabu.


"Mimi sikuwahi kufahamu wala kupata taarifa kama mtoto wangu anaumwa na amepelekwa kutibiwa na wala sikuwa nafahamu anasumbuliwa na ugonjwa gani, kuna siku nilipata taarifa kupitia vyombo vya habari kuwa amefariki lakini taarifa hizo hazikuwa na ukweli," alisema Consolata.

 
Taarifa za awali ambazo zilitolewa na vyombo vya habari kuhusu kifo cha William Mgimwa zilimshtua na kumshangaza mama yake kutokana na kutofahamu nini hasa kimemsumbua mpaka mauti kumfika bila yeye kujua.


Taarifa za uhakika wa kifo cha mwanae ambazo alizipata Januari Mosi alizipokea kwa masikitiko makubwa ukizingatia Mgimwa ndio mwanae wa kwanza lakini pia ni watano katika kupoteza maisha.
Mama huyo alililiambia gazeti hili kuwa alibahatika kupata watoto nane ambapo watatu wapo hai na watano wamefariki dunia.


William Mgimwa ni mtoto wa kwanza katika familia ya mjane huyo na pia alikuwa tegemezi la familia hiyo kutokana na kuwasaidia watoto yatima walioachwa na ndugu zake hao ambao walitangulia mbele za haki.


"William ndiye tegemeo langu kubwa kwa sababu ndiye alikuwa anasaidia familia pamoja na kuwasomesha watoto hawa wa marehemu ndugu zake, sasa hivi sijui ni nani atakaye wasaidia na kuwaendeleza katika elimu," alisema mama huyo.


Hata hivyo marehemu William Mgimwa ameacha mjane mmoja na watoto saba ambapo wakike ni wawili na watano wa kiume ambao walikuwa wakimtegemea kwa kila kitu ili waweze kufanikiwa katika maisha yao ya baadaye.


Kwa upande wake dada wa marehemu Rosemary Mgimwa alisema kuwa kaka yao ndio alikuwa nguzo ya familia hivyo amewaacha pengo kubwa ambalo hawajui watalizibaje kutokana na familia hiyo kuondokewa na kiungo muhimu katika familia hiyo.


"Nimeupokea msiba huu kwa masikitiko makubwa sana kwa sababu awali vyombo vya habari vilitangaza kuwa amefariki dunia tukashangaa kwa sababu hatukuwahi kupata taarifa za ugojwa na hatufahamu alikuwa anaumwa nini,"alisema Rosemary.


Sambamba na hayo mke wa marehemu Jonisia Kakingo pamoja na mdogo wa marehemu Joakim Mgimwa walifika afrika kusini baada ya kupata taarifa za awali kuwa ngugu yao amefariki dunia ndipo wakaamua kwenda wakimuuguza mpaka kufikia kuaga dunia.


Marehemu william Mgimwa alifariki dunia januari mosi majira ya saa tano asubuhi katika hospitali ya Kloof medi-clinic prektoria, nchini afrika ya kusini ambapo alikuwa almelazwa kwa muda akipatiwa matibabu.


Mwili wa maerhemu unatarajiwa kuwasili mjini Iringa leo saa kumi jioni katika uwanjwa wa ndege Nduli na kuagwa katika ukubwi halmashauri ya wilaya ya iringa vijijini ambapo wananchi watatoa heshima zao za mwisho na kuondoka kuelekea kijijini kwao Magunga ambapo maziko yatafanika siku ya jumatatu majira ya saa sita mchana.

 ......................................

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO YA KIFO CHA ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA DKT. WILLIAM MGIMWA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib  Bilal, akisani Kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dkt. William Mgimwa, aliyefariki dunia Januari 01, 2014 huko nchini Afrika ya Kusini alikokuwa amelazwa kwa matibabu. Dkt. Bilal alifika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, jijini Dar es Salaam 3. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mke wa marehemu Dkt. Mgimwa, Jane Mgimwa, wakati alipofika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, jijini Dar es Salaam,  4 5 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia wa marehemu Dkt. Mgimwa, wakati alipofika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, jijini Dar es Salaam, leo  
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, akisani Kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dkt. William Mgimwa, aliyefariki dunia Januari 01, 2014 huko nchini Afrika ya Kusini alikokuwa amelazwa kwa matibabu. Dkt. Bilal alifika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, jijini Dar es Salaam, leo  8. 
Baadhi ya Mawaziri na wabunge waliofika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, leo.

Mwili wa Dkt. William Mgimwa ulivyowasili Kutoka Nchini Afrika Kusini.

Ndege iliyoubeba mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. Willium Mgimwa Ilipowasili katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Leo Kutokea Nchini Afrika Kusini alipokutwa na Mauti siku chache zilizopita.

Mjane Mama Jane Mgimwa(katikati) akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Afrika kusini Radhia Msuya(kulia) mara baada ya kuwasili kutoka nchini Afrika kusini

Naibu Waziri Wizara ya Fedha Saada Mkuya(kulia) akimsindikiza Mke wa Marehemu Mama Jane Mgimwa(katikati)katika chumba cha mapumziko mara baada ya kuwasili katika katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Leo.Kushoto ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mh. Sophia Simba.

Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Wabunge waliojitokeza kuupokea mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Dkt. Willium Mgimwa.

Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue akitoa heshima kwa kugusa Jeneza Lililobeba mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu  Dkt. Willium Mgimwa Katikati ni Waziri wa Ujenzi Mh. John Magufuli na wa Mwisho ni Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mh.Fenella Mukangara.

Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. Willium Mgimwa Ukiingizwa kwenye gari Maalum Tayari kwa ajili ya kuelekea nyumbani kwa marehemu kwa taratibu nyingine za mazishi.


No comments: