Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Mbeya, Leonard Magacha. akiongea na watatibu wa tiba asili kabla yakuwakabidhi vyeti |
Boniventura Malongo Mratibu watiba asili kitaifa akimkaribisha mgeni rasmi |
Mratibu wa vikundi , Zahra Mansour akisoma risala mbele ya mgeni rasmi |
CHET CHA MMOJA WA WASHIRIKI IUTOKA WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA |
Picha ya pamoja
SERIKALI imewaagiza Watabibu wa Tiba
mbadala na Tiba Asili kutojihusisha na matibabu ya ugonjwa wa Ukimwi
kutokana na Madaktari bingwa na wataalamu wa afya kushindwa kugundua dawa za
ugonjwa huo ambapo kufanya hivyo kutaongeza vifo kwa wagonjwa wengi kwa
kukimbilia tiba mbadala na kuacha kutumia dawa za kuongeza nguvu.
Alisema kama kuna mtu ametafiti dawa na
anadhani zinaweza kutibu ugonjwa wa Ukimwi ni bora akazipeleka kwa wataalamu
ili zithibitishwe kwa matumizi ya binadamu kuliko kuanza kuwapa watu hali
itakayoongeza vifo visivyokuwa na lazima kipindi hiki ambacho bado watafiti
wanaendelea kutafuta dawa halisi za kutibu magonjwa hayo.
Agizo hilo lilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa
Mbeya, Abbas Kandoro, wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti vya usajili wa Muda
kwa Watabibu wa tiba asili Mkoa wa Mbeya, iliyofanyika katika ukumbi wa
Mikutano wa Hospitali ya Mkoa, ambapo Mkuu wa Mkoa aliwakilishwa na Katibu
Tawala Msaidizi Mkoa wa Mbeya, Leonard Magacha.
Mbali na hilo Kandoro imeiagiza
pia Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kuhakikisha inatengewa bajeti kwa
ajili ya kuratibu na kufuatilia shughuli zinazofanywa na Matabibu wa Tiba Asili
na tiba mbadala ili kujiridhisha na kazi zake.
Alisema ni vema Ofisi ya Mganga Mkuu wa
Mkoa kutembelea vituo vya Waganga wa Tiba mbadala ili kujiridhisha na kazi zao
kutokana na masharti ya usajili yanayokataza kupiga ramli, uchawi,
ushirikina,mazingaombwe na upigaji ramli chonganishi ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha wote wanaojishughulisha na tiba asili wanakuwa na vibali halali vya
Serikali.
Alisema Serikali imetambua kazi za
Wahudumu wa tiba asili na tiba mbadala na ndiyo maana ikaunda baraza ambalo
lilipewa mamlaka ya kusajili kwa mujibu wa Sehemu ya 4 kifungu cha 14, 16 na 17
cha Sheria ya Tiba asili na mbadala namba 23 ya Mwaka 2002.
Aliongeza kuwa Matabibu wa tiba asili na
mbadala wanatakiwa kujitofautisha na waganga wa kienyeji kwa kuweka mazingira
masafi ya kufanyia shughuli za kitabibu ili kuwa kivutio kwa wananchi na wateja
wao ikiwa ni pamoja na kutoa tiba kwa bei nafuu ili kuwa msaada kwa wagonjwa
wanaoshindwa kumudu gharama za Hospitalini.
Magacha ambaye alimwakilisha Mkuu wa
Mkoa katika Hafla hiyo alisema changamoto inayowakabili wahudumu wa tiba asili
na tiba mbadala ni kukosa ushirikiano na Madaktari wa Hospitali ambao ndiyo
wataalamu zaidi kuliko wao ambapo aliongeza kuwa wakishirikiana na madaktari
itawarahisishia wao kuwatibu vizuri wagonjwa kutokana na vipimo vya Hospitali
badala ya kutibu kwa kukisia.
Katika Hafla hiyo jumla ya Watabibu 46
walikabidhiwa vyeti vya usajili wa Muda kutoka Baraza la Tiba Asili na Tiba
Mbadala, ambapo Mkoa wa Mbeya ukiwa na jumla ya matabibu 3261 ambapo kati yao
waliosajiriwa ni 46 pekee.
Kwa upande wake Chama cha Watabibu Mkoa
wa Mbeya(ATME) katika risala yao kwa Mgeni rasmi iliyosomwa na Mratibu wa
vikundi hivyo, Zahra Mansour walisema miongozo na taratibu zilizopo WAUJ
inayohusu Urasimishaji wa Tiba Asili na Tiba mbadala itolewe kwa wakati kwa
wadau wa tiba asili na Tiba mbadala.
Walisema hotuba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania iliyotolewa Septemba 24, 2010 ya kuzindua urasimishaji
wa tiba asili na tiba mbadala Nchini isambazwe kwawadau wa tiba asili ili itoe
mtazamo wa tiba asili kwa kuweka kwenye vitabu vyote vya mwongozo wa tiba
asili na tiba mbadala sehemu ya utangulizi wa mwongozo.
Pia walisema ni vema idara ya Mkemia
mkuu wa Serikalikupewa ruzuku ili kupunguza gharama za upimaji wa dawa asili
zinazopelekwa na watabibu wa tiba asili kupimwa katika maabara ya Mkemia Mkuu
wa Serikali kama zinafaa kwa matumizi ya mwanadamu.
.................................................................................
MOTO MKUBWA WAZUKA JANCO MOTEL JIJINI MBEYA
|
No comments:
Post a Comment