Sunday, February 2, 2014

DR. JAKAYA KIKWETE AONGOZA MAELFU YA WANANCHI KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 37 YA CCM JIJINI MBEYA

1Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akiwasili kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya tayari kwa kuwaongoza wana CCM na wananchi wa mkoa wa Mbeya katika maadhimisho ya miaka 37 ya Chama Cha Mapinduzi, ambapo viongozi mbalimbali wa serikali na Chama wamehudhuria, maelfu ya wananchi wakiwa wamejitokeza kwa wingi walikuwa wakishangilia kwa nguvu, Dr. Jakaya Kikwete amewahimiza viongozi wa CCM kuiga mfano wa Katibu Mkuu wa chama hicho Ndugu Abdulrahman Kinana kwa kufanya kazi badala ya kukaa ofisini, Mnanatakiwa kuwafuata wanachama waliko na sio kukaa ofisini na kuwa Mamangimeza kauli ambayo Abdulrahman Kinana amekuwa akiirudia mara nyingi kwenye ziara zake katika mikoa mbalimbali. 2Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na  Katibu Mkuu wa chama hicho Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Sokoine. 3Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akizungumza jambo  na  Katibu Mkuu wa chama hicho Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Sokoine, Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula. 4Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akiwapungia mkono wana CCM  na wananchi waliojitokeza katika maadhimisho hayo. 5Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akiendelea kusalimia wananchi kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. 6Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akiwa amenyanyua juu alama ya Nyundo na jembe alama ambayo inatumiwa na Chama cha Mapinduzi ikiwa na maana ya wakulima na wafanyakazi. 7 
Umati wa wananchi ukiwa umejitokeza katika maadhimisho hayo. 8 
Vijana wapatao 37 wakirusha juu njiwa 37 ikiwa ni ishara ya kutimiza miaka hiyo kwa amani 9 
Moja ya kundi la TOT ndogo likitumbuiza katika maadhimisho hayo. 10 
Gwaride la Chipukizi likitoa heshima kwa Mwenyekiti wa Chama chama Mapinduzi Dr. Jakaya Kikwete. 11 
Kiapo cha Utii kwa chama 12 
Heshima kwa chama zikiendelea. 13 
Mwigizaji wa filamu Jacob Steven JB akizungumza kwa niaba ya wenzake kabla  ya waigizaji hao wa Bongo Movie kukabidhiwa kadi zao na Rais Jakaya Kwete kwenye uwanja wa Sokoine leo 14 
Rais Dr. Jakaya Kikwete akipiga picha ya pamoja na wasanii waigizaji wa filamu mara baada ya kuwakabidhi kadi zao kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya leo19 
Nyomi la wananchi likiwa limefurika kwenye uwanja wa Sokoine 23 
Post a Comment