Sunday, February 2, 2014

YANGA YAITANDIKA MBEYA CITY 1-0


yanga_1_f87a7.jpg
Mshambuliaji wa timu ya yanga, Mrisho Ngasa (17) akichuana vikali ili kuwania mpira na beki hodari wa timu ya Mbeya City, Deogratias Julius kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara ambapo timu ya Yanga iliibuka na ushindi kwa kuichapa timu ya Mbeya city goli 1-0, goli la Yanga lilipachikwa na Mrisho Ngasa mnamo dakika ya 15 ya kipindi cha kwanza cha mchezo huo.
yanga_2_0bf7d.jpg
Beki wa timu ya Mbeya City, Deogratias Julius akiondoa mpira katika eneo la hatari kwenye lango la timu hiyo.
yanga_3_0c427.jpg
Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Haroun Niyonzima pamoja na beki wa Mbeya City, Yussuf Abdallah wakichuana vikali kuwania mpira katika mchezo huo wa mzungunguko wa raundi ya pili ya ligi kuu ya Tanzania bara uliochezwa leo katika uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

yanga_4_b12cc.jpg
Mashabiki wa timu ya Mbeya City wakiwa wamefurika uwanjani hapo kuishangilia timu yao.
yanga_5_13657.jpg
Mbuyu Twite wa timu ya Yanga akichomoka na mpira na kumwacha mchezaji wa Mbeya City katika mchezo huo.
yanga_6_c76ba.jpg
Hii ndiyo ilikuwa furaha ya wachezaji wa Yanga baada ya kupata goli la kwanza.
Moja ya basi la mwendo kasi likikatiza mtaa wa Lumumba ikiwa ni sehemu ya majaribio ya mabasi hayo ambayo yanaaminika yataondoa kabisa tatizo la usafiri katika jiji la Dar.

MABASI YA MWENDO KASI YAKIWA MAJARIBIONI DAR


mwendokasi_9b89b.jpg
Moja ya basi la mwendo kasi likikatiza mtaa wa Lumumba ikiwa ni sehemu ya majaribio ya mabasi hayo ambayo yanaaminika yataondoa kabisa tatizo la usafiri katika jiji la Dar.
mwendokasi1_37785.jpg

Post a Comment