







Maaskari wa vikosi vya usalama Barabarabi na Usalama wa rais wakijiweka sawa na kuupanga msafara wa matembezi hayo
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete kulia akiwapungia
mkono wananchi waliojitokeza barabarani wakati matembezi hayo
yakiendelea.


Mwitikio wa wananchi ulikuwa mkubwa pamoja na kwamba matembezi hayo yalianza mapema saa moja na nusu mpaka saa mbili na robo.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete kipenzi cha watoto
ameshiriki nao katika matembezi hayo kama anavyoonekana akitembea
sambamba na watoto


Umati wa wananchi ukiwa umefunika barabara
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete kulia akiingia
kwenye bustani ya jiji la Mbeya tayari kwa kupokea matembezi hayo
yaliyoanzia Soweto Mwanjelwa na mkumalizikia katika bustani hiyo kiasi
cha kilomita tano. kutoka kushoto ni Katibu wa NEC Fedha na Uchumi Mama
Zakhia Megji, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana , Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Godfrey Zambi.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete mara baada ya kupokea matembezi hayo kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Godfrey Zambi na kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula na Marck Mwandosya Waziri Ofisi ya Rais kazi Maalum



Nape
Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akitambulisha viongozi
mbalimbali mara baada ya Rais Dr. Jakaya Kikwete kupokea matembezi hayo
katika bustani ya jiji .

Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe akizungumza na wananchi, kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akiteta jambo na
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kulia na Dr. Mohamed Seif
Khatibu Katibu wa NEC Oganizesheni huku wakifurahia mazungumzo hayo
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akizungumza na wana
Mbeya mara baada ya kupokea matembezi hayo kwenye bustani ya Jiji jijini
Mbeya ikiwa ni maadhimisho ya miaka 37 ya Chama cha Mapinduzi
yanayofanyika kwenye uwanja wa Sokoine leo jijini Mbeya.


No comments:
Post a Comment