Friday, February 7, 2014

HOSPILATALI YA RUFAA MBEYA IKISHIRIKIANA NA KAMPUNI YA BIA TBL IMEANDAA BONANZA LA NGUVU SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 8/2/2014


Katibu wa Hospitali  Aisha Mtanda akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa hospitali ya Rufaa Mbeya 


Mwenyekiti wa kamati ya sherehe Christopher Mwakubombaki moja wa waandaaji wa bonanza hilo

Seraphine Mushi katibu katika kamati hiyo


Baadhi ya waadishi wa habari



Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, katibu wa Hospitali hiyo, Aisha Mtanda alisema kuwa bonanza hilo ambalo litabeba ujumbe usemao,HUDUMA BORA INAWEZEKANA KWA PAMOJA TUMETHUBUTU TUMEWEZA NA TUNASONGA  MBELE.  limeandaliwa na Uongozi wa hospitali hiyo kwa kushirikiana na kampuni ya Bia TBL  na kwamba bonanza hili litafanyika siku ya Jumamosi(February 8, mawaka huu).
Alisema kuwa lengo la bonanza hilo ni kufanya hafla fupi kwa watumsihi wa Hospitali hiyo kwa kuaga mwaka wa 2013 na kuukalibisha mwaka mpya wa 2014, ambalo pia litafanyikia katika viwanja vya Chuo cha Uhasibu (TIA)tawi la Mbeya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa sherehe  Christopher Mwakibombaki alisema katika Bonanza hilo kutakuwa na michezo mbali mbali kama vile mpia wa miguu, mpira wa pete, Netboli, Basketi boli, Voleboli, kuvuta kamba, kukimbia kwenye magunia,kukuna nazi na mashindano ya kula.
Aliongeza kuwa taasisi zinazotarajia kushiriki ni pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Halmashauri ya Jiji, kampuni ya Saruji Mbeya, Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Madiwani wa Halmashauri wa Jiji, Kampuni ya Bia (TBL), Hospitali ya Rufaa na kitengo cha Benki ya damu salama.

Na Mbeya yetu

No comments: