Tuesday, February 25, 2014

KANISA LA KKKT USHARIKA WA MBIGILI KIJIJI CHA NGELENGE WILAYANI RUNGWE MKOA WA MBEYA WAMPOKEA KWA FURAHA ADEN JOSEPH MWAKYONDE BAADA YA KUFANIKISHA UJENZI WA KANISA LA KIJIJI CHA NGELENGE

WAKRISTO WA KIKIJI CHA NGELENGE USHARIKA WA MBIGILI KANISA LA KIIJILI LA KILUTHERI TANZANIA WAMPOKEA KWA FURAHA ADEN JOSEPH MWAKYONDE KIJIJINI PAO BAADA YA KUFANIKISHA UJENZI WA KANISA KIJIJINI HAPO AMBAPO TAREHE 23.10.2013 HARAMBEE ILIFANYIKA KIJIJINI HAPO NA ADEN MWAKYONDE AKIWA MGENI RASIM

IKIWA IMEPITA MIEZI MINNE TU WAKRISTO WA KIJIJI CHA NGELENGE WANA SALI KATIKA KANISA LAO ZURI JAPO CHANGAMOTO ZA SASA NI KUPIGA LIPU NJE NA KUPAKA RANGI NDANI PAMOJA NA KUTENGENEZA SAMANI ZA NDANI YA KANISA HIVYO ADENI MWAKYONDE AMEWATAKA WAKRISTO WA NGELENGE KUWA PAMOJA KATIKA KUMALIZIA CHANGAMOTO ZILIZO BAKIA ILI NENO LA MUNGU KUHUBIRIWA KWA AMANI NA UPENDO KANISANI HAPO

KULIA MCH ASWILE MWASANDUNGILA AKIMPA MKONO WA SHUKRANI ADEN MWA KYONDE KWA NIABA YA WAKRISTO WA KIJIJI CHA NGERENGE

KULIA ADEN MWAKYONDE AKIWASHUKURU WAKRISTO WA KIJIJI CHA NGELENGE KWA MAPOKEZI YAO AMBAYO HAJAWAHI KUYAONA TANGU KUZALIWA KWAKE HIVYO AMEWATAKA WAKRISTO WA KIJIJI CHA NGELENGE KWA PAMOJA KUMSHUKURU MUNGU KWA PAMOJA KWA MAANA KILA KITU KINATOKA MIKONONI MWAKE

KULIA MZEE ANDWELE MWAMPETELE AKIMSHUKURU MUNGU KWA KUFIKA TENA ADEN MWAKYONDE NA ALIOONGOZANA NAO KIJIJINI HAPO NGELENGE MAANA WALIONA BUSARA KUMUALIKA TENA KUJA KUJIONEA UJENZI WA KANISA ULIPOFIKIA BAADA YA KUFANYIKA KWA HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA LA KIJIJI MAANA UWEPO WA KANISA HILO KUNAONDOA USUMBUFU WA KUSAFIRI MWENDO MREFU SANA KWENDA KUSALI KANISA KUU LA USHARIKA HIVYO KANISA HILI LINAWAWEZESHA HATA WASIOJIWEZA KUSALI KARIBU NA MAKAZI YAO

PICHA YA PAMOJA NJE YA KANISA LA KIJIJI CHA NGELENGE WAKIWA NA NYUSO ZA FURAHA NA AMANI HUKU WAKIIMBA NA KUMSIFU MUNGU

IBADA YA SHUKRANI ILIANZIA USHARIKANI KKKT MBIGILI  NA WASHARIKA WALIPATA WASAA WA KUMSHUKURU ALIYEKUWA MGENI RASMI KATIKA HARAMBEE YA KUWEZESHA UJENZI WA KANISA LA KIJIJI CHA NGELENGE USHARIKA WA MBIGILI

BAADHI YA WASHARIKA WAKIWA IBADANI USHARIKA WA MBIGILI

MCHUNGAJI WA USHARIKA AKIWA NA BARAZA LA WAZEE WA USHARIKA WA MBIGILI WAKIMPA JAPO ZAWADI YA UTAMBUA MCHANGO WAKE KWA KANISA KATIKA UJENZI WA KANISA LA KIJIJI CHA NGELENGE  AMBAPO MCHUNGAJI AMESEMA KUWA USHARIKA ULIANDAA MALA NNE HARAMBEE LAKINI HAWAKUFANIKIWA KUKUBALIWA KWA WANAOWAKARIBISHA LAKIN ADEN JOSEPH MWAKYONDE ALIHESHIMU SANA MWALIKO WAO NA KUFANIKIWA KUFIKA NA KUWA CHACHU YA UJENZI WA KANISA AMBAPO LEO TAYARI KANISA LIMEKAMILIKA NA WAKRISTO WANASALIA NDANI

"JAPO KIDOGO LAKINI KANISA LIMEONA TUTAMBUE MCHANGO WAKO" AKISEMA KATIBU WA USHARIKA HUKU AKIMKABIDHI ZAWADI YA KUKU ADEN MWAKYONDE

ADEN JOSEPH MWAKYONDE AKIONGEA NA WAKRISTO WA USHARIKA WA MBIGILI AMESEMA KUWA ALIKUBALI MWALIKO KWAKUWA NI WAJIBU KUMTUMIKIA MUNGU KWAKUWA TU HAI NA VYOTE TULIVYO NAVYO NI MALI YA MUNGU. HUKU AKITOA CHANGAMOTO YA KUANZA UJENZI WA CHOO KANISANI HAPO AMBAPO AMESEMA IFIKAPO SIKU YA HARAMBEE YA MWEZI WA SITA YA UNUNUZI WA GALI LA KANISA KWA AJILI YA HUDUMA  CHOO CHA KISASA KIWE KIMESHAANZA KUTUMIKA

FURAHA MSHUA MWAMBUNGU AKIWA NI RAFIKI ALIYEONGOZANA NA ADEN MWAKYONDE AMEWATAKA WANA MBIGILI KUMTUMIKIA MUNGU KWA MOYO NA UAMINIFU MAANA KANISA NDIO MLEZI WA JAMII KIROHO, KIAKILI NA KIMWILI HIVYO AMEWATAKA  WAKRISTO KUMTUMIKIA MUNGU KWA UAMINIFU

BAADHI YA WAZEE WA USHARIKA WA MBIGILI WAKIWA MAKINI KUSIKILIZA

ENENDENI KWA AMANI YA BWANA
Post a Comment