Thursday, February 6, 2014

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JAKAYA KIKWETE ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA JENGO LA OFISI ZA UTAWALA ZA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA UNOFANYWA NA KIKOSI CHA UJENZI CHA JESHI LA MAGEREZA, MJINI DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea maelezo ya hatua mbalimbali zilizofikiwa katika Ukarabati wa Jengo la Ofisi za Utawala za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania toka kwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Kibwana Kamtande (wa kwanza kushoto) alipotembelea hivi karibuni Mjini Dodoma(wa kwanza kulia) ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda(wa pili kulia) ni Waziri wa Sera na Uratibu wa Bunge. Mhe. William Lukuvi. image_1 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda(katikati) akiwa ameongozana na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Kibwana Kamtande kabla ya kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipotembelea kufanya ukaguzi wa Ukarabati wa Jengo la Ofisi za Utawala za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo Mhe. Rais ameonyesha kuridhishwa na kasi ya ukarabati unaofanywa na Jeshi l Magereza kupitia Shirika lake la Magereza. image_2 
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Kibwana Kamtande(wa kwanza kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza ambao wanasimamia kwa karibu Ukarabati wa Jengo la Ofisi za Utawala za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linalokarabatiwa na Jeshi la Magereza kupitia Shirika lake la Magereza ambapo hivi karibuni Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameridhishwa na kasi ya ukarabati wa Jengo hilo alipotembelea Mjini Dodoma(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza). photo 
Hatua mbalimbali iliyofikiwa  ya ukarabati wa Jengo la Ofisi za Utawala za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililopo Mjini Dodoma ambapo hivi karibuni Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alifanya ukaguzi wa Ukarabati wa Jengo hilo na kurudhishwa na kasi ya Ukarabati huo unaofanywa na Jeshi la Magereza kupitia Kikosi chake cha Ujenzi kilicho chini ya Shirika la Magereza.

No comments: