Monday, February 17, 2014

Wananchi wanaoishi vijiji vya pembezoni mwa ziwa Nyasa wameiomba serikali kutatua haraka suala la usafiri wa meli ili kutatua changamoto zinazowakabili ili kukuza pato lao na Taifa kwa ujumla.


Ziwa Nyasa

Nahodha wa meli ya Mv Songea Thom Faya amekiri kuwepo kwa ubovu wa meli hizo na kuiomba serikali kufanya haraka kuleta meli nyingine ili kuondoa adha ya matengezo ya mara kwa mara ambayo hutumia fedha nyingi na wakati mwingine huwalazimu kwenda nchi jirani ya Malawi kutokana na kukosekana cherezo.


Mizigo ikipandishwa  MeliniZiwa Nyasa


Wananchi wanaoishi  vijiji vya pembezoni mwa ziwa Nyasa wameiomba serikali kutatua haraka suala la usafiri wa meli ili kutatua changamoto zinazowakabili ili kukuza pato lao na Taifa kwa ujumla.

Kauli hiyo wameitoa  katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Matema,Lumbila,Ifungu,Nsisi,Lupingu,Manda,Ndambi na 
Lundu.

Vijiji vingine na pamoja na Nkili,Njambe,Liuli na Mbambabay ambavyo licha ya kuwa na fursa ya kulima na kuvua hawana uhakika wa kuuza bidhaa zao kutokana na ukosefu wa meli ya uhakika kutokana na meli zilizopo  yaani MV Iringa na MV Songea kuchakaa.

Wananc hi hao wamesema kuwa takriblibani kwa majuma matatu meli hizo hazijafanya kazi kutokana na kuharibika hivyo kuleta kero kwa wagonjwa mbalimbali ambao husafirishwa kupitia njia hizo ili kwenda kutibiwa Hospitali ya Wilaya ya Kyela au Rufaa Mbeya.

Kwa upande wake Nahodha wa meli ya Mv Songea Thom Faya amekiri kuwepo kwa ubovu wa meli hizo na kuiomba serikali kufanya haraka kuleta meli nyingine ili kuondoa adha ya matengezo ya mara kwa mara ambayo hutumia fedha nyingi na wakati mwingine huwalazimu kwenda nchi jirani ya Malawi kutokana na kukosekana cherezo.

Aidha Faya amesema kuwa kutokana na ubovu wa mara kwa mara abiria wanahofu kupanda meli hizo na kulazimika kuwa na abiria wachache hivyo kupata hasara kwa shirika na kushindwa kumudu gharama za uendeshaji.

Hivyo ameiomba serikali kutimiza ahadi yake ya Rais Jakaya Kikwete ambapo aliahidi kuleta meli mpya ili kuondoa kero inayowakabili ili kuleta msukumo wa maendeleo kwa wakazi wa mwambao wa ziwa Nyasa ambapo njia pekee na uhakika huegemea meli.

Hivi karibuni Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi[CCM] Abrahamani Kinana alifanya ziara kujionea mwenyewe adha wanayopata wananchi wanaoishi pembezoni mwa ziwa Nyasa ambapo alilazimika kusafiri na meli ya MV Songea kutoka bandari ya Mbamba bay iliyopo wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma kupitia Mkoa wa Njombe hadi bandari ya Itungi wilaya Kyela Mkoani Mbeya na kuahidi ombi lao kulifikisha serikalini kwani ndiyo watekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi.

Na Ezekiel Kamanga 
Mbeya yetu 
Post a Comment