Rais
Jakaya Kikwete anatarajiwa kuhutubia Bunge Maalum Machi 21 mwaka huu
mjini DodomaKauli hiyo imetolewa leo na Katibu wa bunge hilo, Yahya
Khamis Hamad wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa
waandishi wa habari wa ofisi za Bunge mjini Dodoma.
"Kwa
mujibu wa kanuni ya 75 (1), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
atalihutubia Bunge Maalum siku ya Ijumaa Machi 21 ,mwaka 2014 saa
10:jioni, ambapo wageni waalikwa wote watatakiwa kuwa wameingia na
kuketi katika maeneo watakayoelekezwa saa 9:00 alasiri," alisema Katibu
huyo.
Aidha
Katibu huyo alisema ratiba ya shughuli hiyo itaanza na kikao cha Bunge
saa 9:10 na baadae kikao hicho kitaanza saa 9:20 kwa ajili ya kumpokea
Rais.
Aliongeza
kuwa mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge, Rais Kikwete
atapokewa na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu, Naibu Katibu wa
Bunge Maalum, ambapo baadae ataelekea katika jukwaa maalum kwa ajili ya
kupokea salamu za heshima na kukagua Gwaride Maalum ambalo limeandaliwa
na jeshi la polisi.
Baada ya
shughuli zote kufanyika katika viwanja vya Bunge kumalizika, utaratibu
umewekwa kwa viongozi kuingia Bungeni kwa maandamano maalum.
Viongozi
watakaohusika katika maandamano hayo ni Makamu wa kwanza wa Rais wa
Zanzibar ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar na
hatimaye Rais Kikwete ambaye atafuatana na Mwenyekiti wa bunge hilo.
Katibu
huyo aliwataja viongozi wegine walioalikwa kuwa ni viongozi wa kitaifa
na watendaji wakuu kutoka pande zote Muungano, viongozi wa kitaifa
wastaafu,ambao ni marais wastaafu kutoka pande zote za muungano,
mawaziri wakuu wastaafu, waziri kiongozimstaafu na maspika wastaafu.ja
Viongozi wengine ni mama Maria Nyerere, Mama Shadia Karume na Mwenyekiti na wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Wageni
wengine walioalikwa katika utaratibu huo ni taasisi za dini,
zisizozakiserikali, tansia ya habari, vyama vyote vya siasa vyenye
usajili wa kudumu, taasisi za elimu, vyama vya watu wenye ulemavu,
wafanyakazi,wafugaji,wavuvi, wakulima na wawakilishi kutoka sekta
binafsi.
Kwa
mujibu wa ratiba ya shughuli hiyo Rais Kikwete anatarajiwa kuhutubia
bunge hilo kwa muda wa saa moja. Hivyo shughuli hizo zitakamilika majira
ya saa 12:00jion
No comments:
Post a Comment