Taarifa hii inatoa mwelekeo wa mifumo ya hali ya hewa, joto na mvua katika kipindi cha miezi ya Juni hadi Agosti (JJA) 2014.
1. MIFUMO YA HALI YA HEWA
Mifumo ya hali ya hewa inaonesha
uwezekano wa kuongezeka kwa joto la bahari katika eneo la ukanda wa
Tropiki la bahari ya Pasfiki kwa kipindi cha miezi ya Juni hadi Agosti
2014. Ongezeko kidogo la joto linatarajiwa katika ukanda wa magharibi ya
bahari ya Hindi. Aidha joto katika bahari ya Atlantik linatarajiwa kuwa
chini ya wastani. Hali hiyo inatarajiwa kusababisha upepo kuvuma kutoka
magharibi ukielekea mashariki katika maeneo mengi ya nchi. Joto la
bahari la juu ya wastani linatarajiwa katika eneo la ncha ya kusini ya
bara la Afrika hivyo kuathiri msukumo wa upepo wa kusi katika kipindi
cha miezi ya Juni hadi Agosti2014. Hali hii inatarajiwa kusababisha
hali ya baridi katika kipindi hicho. Aidha, vipindi vifupi vya mvua za
vinatarajiwa katika maeneo machache ya ukanda wa Ziwa Viktoria, ukanda
wa pwani na katika maeneo ya miinuko.
2: VIWANGO VYA CHINI VYA JOTO NA MVUA: JUNI HADI AGOSTI, 2014
2.1 MATARAJIO YA VIWANGO VYA CHINI VYA JOTO KWA MIEZI YA JUNI HADI AGOSTI 2014
Kindi cha mwezi Juni hadi Agosti, maeneo mengi ya nchi yanarajiwa kuwa makavu na yenye hali ya baridi katika majira haya ya kipupwe.
Mifumo ya hali ya hewa inaonesha kuwa na hali ya joto la wastani katika
kipindi cha miezi ya Juni hadi Agosti 2014 katika maeneo mengi. Aidha,
izigatiwe kuwa hali ya baridi inatarajiwa zaidi nyakati za usiku hadi
mapema asubuhi. Matarajio ya viwango vya chini vya joto katika kipindi
hicho ni kama ifuatavyo:
Ukanda wa ziwa Victoria (Mikoa ya Mwanza, Mara, Chato, Kagera, Shinyanga na Simiyu)
Hali ya joto inatarajiwa kuwa juu ya wastani(Juu ya nyuzi joto 17.2 0C)
katika maeneo mengi. Hata hivyo, katika maeneo ya kusini ya mikoa ya
Shinyanga na Simiyu hali ya joto inatarjiwa kuwa chini ya wastani.
Ukanda wa pwani ya kaskazini
(Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani, maeneo ya kaskazini ya mkoa wa
Morogoro pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba)
Hali ya joto inatarajiwa kuwa juu ya wastani(Juu ya nyuzi joto 22.9 0C) katika maeneo mengi. Hata hivyo, katika maeneo ya miinuko ya mkoa wa Tanga hali ya joto inatarajiwa kuwa chini ya wastani(Chini ya nyuzi joto 15.9 0C).
Ukanda wa nyanda za juu kaskazini mashariki (Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara)
Hali ya joto inatarajiwa kuwa ya wastani(Kati ya nyuzi joto 13.0 0C na 15.8 0C) katika maeneo mengi. Hata hivyo, katika maeneo ya miinuko viwango vya joto vinatarajiwa kuwa chini ya wastani(Chini ya nyuzi joto 13.0 0C).
Ukanda wa magharibi (Mikoa ya Kigoma, Tabora na Katavi)
Hali ya joto inatarajiwa kuwa ya wastani(Kati ya nyuzi joto 14.9 0C na17.0 0C)
katika maeneo mengi. Hata hivyo, katika maeneo ya kaskazini ya mkoa wa
Kigoma (Kibondo) hali ya joto inatarajiwa kuwa ya wastani(Juu ya nyuzi joto 17.0 0C).
Ukanda wa kati (Mikoa ya Singida na Dodoma)
Hali ya joto inatarajiwa kuwa ya wastani(Kati ya nyuzi joto14.1 0C na 14.7 0C ) katika maeneo mengi. Hata hivyo, vipindi vya upepo mkali wenye kuambatana na baridi vinatajiwa katika maeneo hayo.
Ukanda wa pwani ya kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi)
Hali ya joto inatarajiwa kuwa juu ya wastani(Juu ya nyuzi joto 19.10C) katika maeneo mengi.
Ukanda wa kusini (Mkoa wa Ruvuma)
Hali ya joto inatarajiwa kuwa chini ya wastani(Chini ya nyuzi joto 11.80C)
hususan maeneo ya magharibi mwa mkoa wa Ruvuma(Songea na mwambao wa
Ziwa Nyasa). (Aidha, viwango vya joto la wastani vinatarajiwa kwa maeneo
mengine ya ukanda wa kusini.)
Ukanda wa nyanda za juu kusini-magharibi (Mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe pamoja na maeneo ya kusini ya mkoa wa Morogoro)
Hali ya joto inatarajiwa kuwa ya baridi kali ambapo viwango vya joto vinatarajiwa kuwa chini ya wastani(Chini ya nyuzi joto 6.00C). Hata hivyo, katika maeneo ya kaskazini ya mkoa wa Iringa hali ya joto inatarajiwa kuwa ya wastani.

No comments:
Post a Comment