Monday, July 21, 2014

NAPE : CCM HAIKATAZI MWANACHAMA WAKE KUTANGAZA NIA YA KUGOMBEA UONGOZI


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye amesema Chama Cha Mapinduzi hakimzuii mwanachama yeyote kutangaza nia ya kugombea Uongozi katika muhula unaofuata isipokuwa Chama kimezuia kampeni za mapema kwani ndio chanzo cha makundi ndani ya Chama akizungumza kwenye kipindi cha Baragumu kinachorushwa na Channel 10 ,Nape  alisema taratibu za kugombea Uongozi ndani ya chama zipo na kuna Kanuni mbili, moja ni ya Kanuni za Viongozi na Maadili na pili Kanuni zinazosimamia Uchaguzi ndani ya CCM, akinukuu kutoka kwenye kitabu cha Kanuni za Viongozi na Maadili ,Nape alisema “Wanachama wenye nia ya kugombea nafasi ya uongozi katika muhula unaofuata anaweza kutangaza nia ya kugombea lakini haruhusiwi kufanya kampeni kabla ya muda”.
   Akizungumzia juu ya adhabu wanazopewa waliokiuka alisema adhabu hizi zina shabaha ya kuwasaidia wanachama na Viongozi kujirekebisha.
Nape pia alizungumzia suala zima la upatikanaji wa Katiba Mpya,alisema CCM imeshikamana sana kiasi cha kuwachanganya Wapinzani, aliendelea kwa kusema Kanuni,Sheria zinazotumika ni makubaliano ya wote.(Wapinzani walishiriki katika kamati kutengeneza kanuni na sheria na zikapitishwa Bungeni wakiwemo na Rais akasaini).

No comments: