Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akimkabidhi miche bora ya kahawa mkulima mdogo Bi Dorothea Komba wakati
alipolitembelea na kukagua shamba la kahawa AVIV Farm linalomilikiwa na
kampuni ya Olam katika kijiji cha Lipokela wilayani Mbinga, mkoani
Ruvuma leo.Kampuni ya Olam imepanga kutoa jumla ya miche milioni tatu
kwa wakulima wadogo elfu mbili katika vijiji vinne vinavyozunguka shamba
hilo katika kipindi cha miaka mitano ili kuwashirikisha kuzalisha
kahawa bora.
Meneja wa Shamba la Kahawa la AVIV
Farm linalomilikiwa na kampuni ya Olam Bwana Medappa Ganapati
akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mche bora wa kahawa iliyozaa
vyema wakati Rais alipolitembelea na kukagua shamba la kahawa katika
kijiji cha Lipokela, wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma leo

akikata utepe kufungua Soko la Kimataifa la Mkenda lililopo katika kijji
cha Mkenda Mpakani mwa Msumbiji na Tanzania leo.kulia ni mbunge wa
Peramiho Mh.Jenister Mhagama.Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi
Mkoani Ruvuma(picha na Freddy Maro)
No comments:
Post a Comment