Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Marehemu mwenyekiti mstaafu wa
tume ya Uchaguzi JAJI Lewis Makame enzi za uhai wake alipokuwa amelazwa
katika hospitali ya AMI iliyoko Mikocheni jijini Dar es Salaam leo.
ALIYEKUWA
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Lewis Makame,
amefariki dunia katika Hospitali ya Ami Trauma Centre iliyopo Masaki
jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa kwa maradhi yaliyokuwa
yakimsumbua.
Jaji
Makame alifariki jana mchana katika hospitali hiyo, alikokuwa amelazwa
ambapo pia Rais Jakaya Kikwete, alimtembelea kumjulia hali. Taratibu za
mazishi zilikuwa zikiendelea jana nyumbani kwake Masaki.
Historia
fupi iliyopatikana, inaonesha kuwa Jaji Makame alikuwa na Shahada ya
Kwanza ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha London nchini Uingereza, ambapo
baada ya kufanya mazoezi na kufanya kazi nchini humo, alirejea nchini
Tanzania miaka ya 1960 na kutumikia Taifa mpaka alipofikia cheo cha Jaji
wa Mahakama ya Rufaa.
Mbali na
cheo hicho, Jaji Makame pia alitumikia Taifa katika nafasi ya Mwenyekiti
wa NEC na Mwenyekiti wa Jukwaa la Tume za Uchaguzi za Nchi Wanachama wa
Jumuiya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-ECF).
Wakati
akiwa Mwenyekiti wa NEC kwa takribani miaka 19, Jaji Makame aliweka
historia ya kusimamia uchaguzi kadhaa wa vyama vingi nchini.
Alistaafu wadhifa huo baada ya mkataba wake kuisha Julai mwaka 2011. Nafasi yake ilichukuliwa na Jaji mstaafu Damian Lubuva.
No comments:
Post a Comment