Mh Msigwa |
mbunge
mchungaji Msigwa kushoto akiwa na mbunge Chiku Abwao katika moja kati
ya vikao vya baraza la madiwani Manispaa ya Iringa
Na Francis GodwingaBlog
KAMATI
ya uchaguzi wa mkuu wa wilaya ya Iringa mjini kupitia chama cha
Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) imemuengua katika kinyang’anyiro cha
uenyekiti wa wilaya hiyo mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji
Peter Msigwa ambae ndie alikuwa wenyekiti anayemaliza muda wake kwa
kukosa sifa ya kutetea tena nafasi hiyo.
Hatua
hiyo ya kuenguliwa kwa Msigwa imekuja baada ya wajumbe kulalamikia
hatua ya chama kushindwa kulipa kodi ya ofisi ya kata na ile ya wilaya
pia ugomvi mkubwa uliopo kati ya mbunge Msigwa na mbunge mwenzake wa
viti maalum mkoa Chiku Abwao aliyekuwa akigombea nafasi ya kiti mkoa wa
Iringa nafasi ambayo msigwa pia alitangaza kugombea .
Hivyo
kutokana na mvutano huo kamati hiyo iliyoketi usiku wa leo ukumbi
wa Sambala mjini hapa ililazimika kuchukua uamuzi mgumu wa kufyeka
majina ya wabunge hao kugombea nafasi hizo ili kunusuru chama.
Mmoja
kati ya makada wa ambae alishiriki kikao hicho cha kumuengua Msigwa na
Chiku alisema kuwa chanzo cha msigwa kuenguliwa ni kutokana na
kuendekeza kukuza makundi ndani ya chama na kuwa mbali na chama zaidi ya
kufanya chama kuendelea kukosa heshima.
Makundi hayo yanaelezwa kukiwekwa rehani chama hicho wakati kikijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Pamoja
na Mchungaji Msigwa, taarifa hizo zimesema Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa
wa Iringa, Chiku Abwao (Chadema) naye ameenguliwa kuwani nafasi yoyote
ya uongozi katika chama hicho mkoani hapa.
Hivikaribuni
Abwao alinukuliwa akitangaza kuwania nafasi ya uenyekiti wa mkoa wa
chama hicho unaotarajia kufanyika Jumapili keshokutwa.
Kuenguliwa
kwa Msigwa katika uchaguzi huo kumeacha kampuni wagombea wawili
wanaomenyana katika nafasi hiyo itakayosaidia kutoa picha ya jinsi mambo
yatakavyokuwa wakati wa mchakato wa kumpata mgombea ubunge jimbo la
Iringa Mjini mwaka 2015.
Wagombea
hao ni Frank Nyalusi anayeelezwa kuwa ni mfuasi wa kufa na kupona wa
Mchungaji Peter Msigwa na Mohamed Makuke ambaye ni mfuasi wa kundi la
wengi linalodaiwa kumpinga Mchunngaji Msigwa.
Kundi
linalojiita la wengi katika chama hicho limesikika likisema mara kwa
mra kwamba tabia ya Mchungaji Msigwa ndani ya chama hicho inawaweka
katika wakati mgumu wa kutetea nafasi ya ubunge mwaka 2015.
Mchungaji
Msigwa ni kiongozi asiyeambilika, anayejua kila kitu, mbishi, kaidi,
mwenye kiburi, asiyependa watu, mwenye visasi, majivuno na asiyetaka
ushirikiano toka kwa wenzake, asiye na mikakati ya kujenga chama huku
akiamini siasa za kitaifa pekee anazopenda zaidi zinaweza kulinusuru
jimbo hili katika Uchaguzi Mkuu wa mwakani.
Wakati
Mchungaji Msigwa akirushiwa lawama zote hizo, taarifa za uhakika
zimedai kwamba ofisi ya wilaya ya chama hicho imefungwa na wameamuliwa
kuondoka baada ya uongozi wa mbunge huyo unaomaliza muda wake kushindwa
kulipa kodi ya pango. Mchungaji Msigwa ndiye Mwenyekiti wa Chadema jimbo
la Iringa Mjini anayemaliza muda wake hii leo.
Wanachama
wa chama hicho wamechukizwa kwa hatua ya mbunge wao kuridhia kupoteza
ofisi pekee ya chama hicho mjini Iringa kwasababu ya kushindwa kulipa Sh
540,000 walizokuwa wakidaiwa.
Kwa
upande wake mbunge Msigwa alinukuliwa na mwandishi wa habari hizi
akimrushia maneno mmoja kati ya viongozi wa chama hicho kuwa watu
wanamchafua kwa suala la ofisi na kuwa ni ruksa kwa wanachama ambao
wanapenda vyama vyenye ofisi kuhama chadema na kujiunga na vyama
hivyo .
Huku
mbunge Chiku Abwao amethibitisha kuenguliwa kwao katika nafasi hizo
japo amedai kwa upande wake kaonewa na ataendelea kutumia vikao
kuomba kurejeshwa kwa jina lake.
No comments:
Post a Comment