Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda, hivi karibuni
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda amekatiza kwa muda, ziara yake katika Falme za
Kiarabu kwa maelezo kwamba ameitwa nyumbani na Rais Jakaya Kikwete kwa
shughuli maalumu.
Waziri
Mkuu ambaye yuko katika ziara ya kutembelea nchi za Falme za Kiarabu,
ikiwa ni sehemu ya kudumisha ushirikiano na kutafuta wawekezaji,
amekatisha ziara hiyo siku mbili baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,
Jaji Frederick Werema kujiuzulu kutokana na kashfa ya Escrow.
Werema
alijiuzulu juzi na Rais Kikwete akaridhia hatua hiyo, huku umma
ukisubiri hatua zaidi dhidi ya mawaziri na watendaji wa Serikali
waliotajwa katika sakata hilo.
Katika
barua yake ya kujiuzulu, Jaji Werema alisema ushauri wake wa kisheria
kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow haukueleweka na hivyo kuchafua hali ya
hewa.
Kwa
mujibu wa ratiba ya ziara hiyo, leo Waziri Mkuu alitarajiwa kufanya
mazungumzo na washiriki wa maonyesho ya B2B pamoja na kutembelea maeneo
mengine lakini ziara hiyo imefutwa na badala yake anaondoka asubuhi
kurudi nyumbani.
Baadaye leo Pinda alitakiwa kwenda Doha, Qatar kwa ziara kama hiyo hadi Desemba 23.
Baada ya kukamilisha jukumu aliloitiwa, Waziri Mkuu anatarajiwa kurejea Falme za Kiarabu Jumamosi kuendelea na ziara yake.
No comments:
Post a Comment