MATOKEO
ya awali yaliyopatikana mkoani Mbeya katika uchaguzi wa Serikali za mitaa
unaonesha Chama Cha Mapinduzi(CCM) kuongoza katika maeneo mengi
kikifuatiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Akizungumzia
matokeo ya awali,Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya Mwangwi Kundya alisema mpaka
anazungumza na waandishi wa habari,matokeo yalipatikana kwenye vitongoji 2047
kati ya 2567, vijiji 606 kati ya 771 na mitaa 252.
Alisema
kwa upande wa vijiji vya Wilaya ya Chunya yenye vijiji 86 yalikuwa
yamepatikana matokeo ya vijiji 74, ambapo kati ya vijiji hivyo,CCM
ilikuwa imeshinda vijiji 67 na Chadema vijiji saba.
Wilaya
ya Ileje yenye jumla ya vijiji 71 ambapo matokeo yalikuwa yamepatikana ya
vijiji 32 CCM ilikuwa imeshinda vijiji 23 na Chadema vijiji 9.
Kwa
wilaya ya Kyela yenye jumla ya vijiji 93 ambayo matokeo ya vijiji vyote
yalikuwa yamepatikana CCM imeshinda vijiji 79 na Chadema vijiji 13 huku kijiji
kimoja uchaguzi ukiwa haukufanyika.
Wilayani
Mbarali kuliko na jumla ya vijiji 102, matokeo yalikuwa yamepatikana ya Vijiji
97 ambapo CCM ilikuwa imeshinda katika vijiji 81 na Chadema vijiji 16 na
vijiji vitano yalikuwa yakisubiriwa.
Wilaya
ya Mbozi yenye vijiji 125 ambapo matokeo ya vijiji 92 yalikuwa yamepatikana CCM
ilikuwa imeshinda katika vijiji 84,Chadema vijiji 8 na vijiji 33 yalikuwa
yakisubiriwa.
Wilaya
ya Rungwe yenye vijiji155,matokeo ya vijiji 150 yalikuwa yamepatikana,CCM
ilishinda vijiji 127,Chadema vijiji 22,CUF kijiji kimoja na vijiji vitano
matokeo yalikuwa yanasubiriwa.
Wilaya
ya Momba ina vijiji 72 kati ya hivyo vijiji 67 yalikuwa yamepatikana,CCM
ilikuwa imeshinda katika vijiji 43,Chadema vijiji 24 na vijiji vitano yalikuwa
yanasubiriwa.
Kwa
upande wa Mitaa Mbeya mjini kuliko na mitaa 181,CCM imeshinda mitaa 106,Chadema
mitaa 71 na Nccr Mageuzi mtaa mmoja wakati katika mji mdogo wa Tunduma wilayani
Momba ulio na mitaa 71 Chadema iliibuka kidedea katika mitaa 46 na CCM
ikaambulia mitaa 25.
Kwa
upande wa Vitongoji,Chunya yenye vitongoji 438 ambapo matokeo ya vitongoji 288
yalikuwa yamepatikana,CCM ilikuwa imeshinda vitongoji 270 na Chadema vitongoji
18.
Kyela
yenye vitongoji 469 CCM ilikuwa imeshinda vitongoji 377 na Chadema vitongoji 88
huku vitongoji vinne uchaguzi ukiwa unapaswa kurudiwa.
Wilaya
ya Mbozi yenye jumla ya vitongoji 664 ambayo matokeo ya vitongoji 414 yalikuwa
yamepatikana,CCM ilikuwa imeshinda vitongoji 359,Chadema vitongoji 55 na
matokeo ya vitongoji 250 yalikuwa yanasubiriwa.
Wilaya
ya Rungwe yenye jumla ya vitongoji 694,matokeo ya vitongoji 634 yalikuwa
yamepatikana na CCM ilikuwa imeshinda vitongoji 557,Chadema vitongoji 110,Cuf
vitongoji viwili na TLP kitongoji kimoja na vitongoji 60 yalikuwa yakisubiriwa.
Wilaya
ya Momba ina jumla ya vitongoji 302 kati ya hivyo vitongoji 242 matokeo
yalikuwa yamepatikana ambapo CCM ilikuwa imeshinda 189,Chadema 53 na vitongoji
60 vilikuwa bado matokeo yakisubiriwa.
MATOKEO ZAIDI YA UHAKIKA YANAWAJIA
KINGOTANZANIA - 0752881456
|
No comments:
Post a Comment