Tuesday, December 16, 2014

RAIS DKT.JAKAYA MRISHO KIKWETE ATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA MAMA MZAZI WA KULWA,DOTTO NA NICO MWAIBALE, MWILI WASAFIRISHWA LEO KWENDA KIWIRA WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA KWA MAZISHI

 
 Kulia ni Kulwa na kushoto ni Dotto Mwaibale wakiwa na sura za Majonzi wakati wa Ibada fupi ya Kumuombea Mama yao Mpendwa kabla ya kuanza Safari ya kwenda Mbeya
Wa kwanza Kulia ni Mdogo wao wa Mwisho wa Akina Mwaibale Ambwene  na wa pili kutoka kulia ni Dada yao Mkubwa wa akina Mwaibale  Mary Anyitike ambaye ni Kamishna Mkuu Msaidizi wa Skauti  Shughuli za Vijana
Taifa
 
 Mwili wa Marehemu Bi. Twitikege Mlagha Mfumu mama yao Dotto, Kulwa na Nico Mwaibale ukiwa unaandaliwa tayari kwa kuombewa, Kuagwa na kusafirishwa
 Mchungaji Ephraim Mwakajwanga Akiwa anaongoza Ibada ya Kumuaga Mama mzazi wa Dotto, Kulwa na Nico Mwaibale  Bi. Twitikege Mlagha Mfumu leo katika Hospitali ya Temeke
 Baba Mchungaji Ephraim Mwakajwanga wa kanisa la Moravian Kijichi akitoa Neno la Kiroho (Mahubiri mafupi) wakati wa kuuaga Mwili wa Marehemu, Katika Mahubiri hayo alisisitiza kuwa Duniani tunapita kila kitu kinabaki hivyo ni vizuri kila mmoja ajiandae  na kuwa mama ametangulia na sisi tunafuata hivyo yatupasa kuwa tayari
 Meneja Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers Abdalah Mrisho akitoa salam za Rambi rambi kwa wafiwa ambapo Kulwa Mwaibale anafanyia kazi hapo.
Joachim Mushi akisoma utaratibu na kutoa maelezo mbalimbali wakati wa shughuli za kuuaga mwili wa Marehemu.
 Muwakilishi kutoka Jambo Concept ambao ndio wachapishaji wa Gazeti la Jambo leo ambapo Dotto Mwaibale anafanyia kazi huko Mkurugenzi Beny Kisaka wakitoa salam za Rambi rambi ambapo walitoa mkono wa pole wa kiasi cha Shilingi Laki tano.

 Msemaji wa kwa Niaba ya Familia Noah Mwakalasya  akitoa neno la Shukurani kwa niaba ya wanafamilia na kushukuru kwa moyo waliojitolea kuja kumsindikiza mama yao mpendwa
Dada Mkubwa wa akina Mwaibale  Mary Anyitike ambaye ni Kamishna Mkuu Msaidizi  wa Skauti Shughuli za Vijana Taifa akisoma wasifu wa Marehemu mama yao
 Baba Mchungaji Ephraim Mwakajwanga wa kanisa la Moravian Kijichi akitoa Neno la Mbaraka wakati wa kumaliza ibada ya kumuombea Marehemu Mama yao Kulwa, Dotto na Nico Mwaibale kabla ya kuanza safari kuelekea Mbeya kwa Mazishi.
 Mdogo wa Mwisho wa akina Mwaibale Ambwene  akitoa salam za Mwisho kwa Marehemu mama yake
 Dada Mkubwa wa akina Mwaibale Mary Anyitike ambaye ni Kamishna Mkuu Msaidizi  wa Skauti Shughuli za Vijana Taifa akitoa salam za Mwisho za kuuaga mwili wa Marehemu Mama yao
Kulwa na Dotto Mwaibale wakiuaga Mwili wa Marehemu mama yao
 Kulwa Mwaibale akiwa ameshikiriwa na ndugu zake Baada ya Kuaga Mwili wa Mama yake
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers Eric Shigongo na Mkurugenzi wa blog ya Fullshangwe Bw. John Bukuku wakiwa wakiaga Mwili wa Marehem.
 
 
Waombolezaji wakiwa katika Shughuli ya Kuuaga mwili wa Mama yao Dotto,Kulwa na Nico Mwaibale 
******
Rais wa Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete atuma salamu za Rambirambi kwa
Familia ya Mwaibale Kwa kuondokewa na Mama  Mzazi wao mpendwa Bi.Twitikege Mlagha Mafumu
aliye fariki majira ya saa 5 usiku siku ya jumamosi wakati akikimbizwa
hosipitali ya hindra kwaajiri ya Matibabu
Akiwasilisha salaamu
hizo kwaniaba ya Rais Jakaya Kikwete Meneja Mkuu wa Globabal Publishers Limited
Abdalah Mrisho Ameweza  kutoa pole  kwa wafiwa wote kwa ujumla wakiwakilishwa na
Kulwa,Dotto na Nico Mwaibale Hivyo Kuwa na Moyo wa uvumilivu katika kipindi
kigumu kilicho wafika familia ya Mwaibale
Vilevile Aliweza
simama Kwa niaba ya Wanahabari Abdalah Mrisho aliweza kufikisha salaamu hizo
Kwa kuwapa pole familia na wote walio guswa na msiba wakiwemo ndugu,jamaa na
marafiki wa ndugu yetu mpendwa ambaye kwa sasa ni marehemu Bi. Twitikege Mlagha
Mafumu
Mwili wa ndugu yetu
Mpendwa  umeagwa leo Mchana majira ya saa
6 katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke na kuanza safari  ya kuusafirisha kwa kwenda  kumpumzisha
mama mpendwa katika kijiji cha Kibumbe Kiwira mwakenja,Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya  ambapo Anatarajiwa kuzikwa  kesho Tar 17 alasil mwezi wa kumi na mbili
(12) Mwaka huu
Tunapenda kutoa pole
kwa wafiwa wote na Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema peponi 
Amen
Post a Comment