Sunday, January 11, 2015

PICHA: MBUNGE WA MBEYA MJINI MH. JOSEPH MBILINYI APATA AJALI JANA ENEO LA KITONGA.

Mr. Sugu akiwa anapata matibabu Hospitali.
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi akifanya mawasiliano kwa ndugu na jamaa mara baada ya kupata ajali mbaya na kunusurika kifo,ajali hiyo imetokea eneo la Mlima Kitonga Mkoani Iringa .kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa Mh. Mbilinyi alikuwa safarini akitokea Mkoani Mbeya kuelekea jijini Dar akiwa na jamaa zake Wanne katika gari hilo lenye namba za usajili T 148 BQE. katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha.
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi (watatu kushoto) akizungumza namna hali ilivyokuwa mpaka kupata ajali hiyo.
Gari hiyo inavyoonekana.
Picha kwa hisani ya SufianiMafoto.com

No comments: