Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akipokelewa na baadhi ya
watendaji kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Kanda ya Ziwa na
Nishati na Madini mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa
Mwanza. Profesa Muhongo anafanya ziara katika mikoa ya Simiyu, Tabora na
Shinyanga lengo likiwa ni kukagua miradi ya umeme vijijini
inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na
Taneesco.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akisaini kitabu cha
wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega kabla ya kuanza ziara
katika wilaya hiyo ili kujionea utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini
pamoja na kuzungumza na wananchi.
Mkazi
wa kijiji cha Ihale kilichopo wilayani Busega mkoani Simiyu ambaye
jina lake halikupatikana mara moja akiuliza maswali mbele ya Waziri wa
Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na wananchi (hawapo
pichani) mara Waziri alipofanya mazungumzo na wananchi wa kijiji hicho
ili kusikiliza kero zao.
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo kwenye
mkutano na wananchi wa kata ya Ijitu iliyopo wilayani Busega
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akitoa maelekezo
kwa Meneja wa Tanesco- Kanda ya Ziwa Mhandisi Joyce Ngahyoma ( wa mwisho
kushoto) ya kuitaka Tanesco kuongeza kasi ya usambazaji wa umeme
vijijini.
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo
katika mkutano wake na wananchi wa kijiji cha Bushigwamala wilayani
Busega (hawapo pichani)Sehemu ya umati wa wananchi wa kata ya Kalemala
wilayani Busega waliojitokeza kwenye mkutano na Waziri wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter Muhongo wakifuatilia kwa makini hotuba yake.
Meneja
wa Tanesco- Kanda ya Ziwa Mhandisi Joyce Ngahyoma, akifafanua jambo
mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na
wananchi wa kijiji cha Nyamikoma wilayani Busega (hawapo pichani)
Diwani
wa Kata ya Ijitu iliyopo wilayani Busega Vumi Magoti akielezea kero za
umeme katika kata yake mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa
Sospeter Muhongo ( wa pili kutoka kushoto), viongozi na wananchi (hawapo
pichani)
Waziri wa Nishati na Madini Profesa
Sospeter Muhongo (kulia) akitoa maelekezo kwa mtaalamu kutoka kampuni ya
Symbion iliyopewa kazi ya kujenga miundombinu ya umeme katika kijiji
cha Nyamikoma kilichopo wilayani Busega Bw. Steve Thomson (kushoto)
No comments:
Post a Comment