Monday, February 2, 2015

CCM KATIKA PICHA; DR. JAKAYA KIKWETE: MBALI YA HAWA WALIOJITANGAZA WANA CCM WENYE SIFA YA KUGOMBEA URAIS WAKO WENGI, DIAMOND ATIKISA SONGEA

1aMwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh. Said Mwambungu wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Songea tayari kwa kuwaongoza wana CCM na wananchi wengine katika maadhimisho ya miaka 38 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi CCM yaliyofanyika kwenye uwanja wa Majimaji Mjini Songea mkoani Ruvuma , yakihudhhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM na viongozi wa vyama kutoka nchi kadhaa ikiwemo Uganda, Katika maadhimisho hayp Jakaya Kikwete akiwahutubia amewaasa viongozi kutopokea fedha za moto kwani zinaweza kuwaunguza na akaongeza kwamba CCM ni chama chenye hazina ya viongozi mbali ya waliojitangaza kuwania uongozi katika mwaka huu wa uchaguzi lakini pia kuna watu wenye sifa za urais lakini hawajatangaza na hakuna dhambi kama wana CCM watawafuata na kuwaomba wagombee urais ili kuongoza nchi yetu.
Kutoka kushoto wengine ni Ndugu Abdulrahman Kinana Katibu Mkuu wa CCM, Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda na Makamu Mwenyekiti wa CCM Mzee Philip Mangula 2aMwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akiongozana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Songea mkoani Ruvuma. 3aMwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Songea mjini Bw. Joseph Mkirikiti wakati alipowasili mkoani humo kwa ajili ya kushiriki maadhimisho ya miaka 38 ya CCM kushoto ni Mh. Said Mwambungu Mkuu wa mkoa wa  4aMwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akitaniana na Mbunge wa jimbo la nyasa Mh. Kapteni John Komba. 5aMwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na wakuuu wa vyombo vya ulinzi na usaliama wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege Songea mkoani Ruvuma 6aMwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akiangalia ngoma mbalimbali zilizokuwa zikitumbuizwa na vikundi mbalimbali vilivyompokea leo kwenye uwanja wa ndege wa Songea mkoani Ruvuma.22 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara na Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi Mh Mwigulu Nchemba akipokelewa na Nape nnauye Katibu wa Itikadi na Uenezi wakati alipowasili kwenye uwanja wa Majimaji. 9a
Star Tv wanastahili kupongezwa kwa kazi waliyoifanya leo kwani kazi yao ilikuwa imetulia na imepongezwa na watu wengi waliokuwa wakifuatilia kwenye luninga huyu ni mmoja wa wapigapicha wa kituo hicho akifanya vitu vyake.  13a 
Baadhi ya wazee waliofika kwenye maadhimisho hayo wakipelekwa eneo la kukaa. 14a 
Mzee Philip Mangula Makamu Mwenyekiti wa CCM bara katikati, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi Dr. Emmanuel Nchimbi na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakimsubiri Mwenyekiti wa chama hicho Dr. Jakaya Kikwete kuwasili. 15aMwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akiwasili kwenye uwanja wa Majimaji huku akiwapungia mikono wana CCM na wananchi aliojitokeza katika maadhimisho hayo yaliyofana. 1617aMwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa majimaji. 18Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akivishwa skafu na vijana wa chipikizi mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea. 19aMwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akipokea heshima kwa kuimbiwa wimbo wa taifa na vijana wa chipukizi. 20a 
Gwaride la heshima likipita mbele ya jukwaa kuuu na kutoa heshima. 27a 
Mpiganaji wa kituo cha Televisheni cha Star TV akifanya vitu vyake katika katika maadhimisho hayo. 29a  
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi NDugu Nape Nnauye akizungumza jambo katika maadhimisho hayo32a 
Umati wa watu waliojitokeza katika maadhimisho hayo. 33a 34a 
Kapteni John Komba kulia na Abdul Misambano wa TOT wakiimba katika maadhimisho hayo 35a 36a 
Mkuu wa wilaya ya Songea mjini Mh. Joseph Mkirikiti akiwapooza wananchi wa Songea kutulia ili Diamond Plutnamz kufanya vitu vyake jukwaani.

No comments: