Monday, February 2, 2015

WASWASI WA MAUAJI YA WATOTO KUANZA TENA MJINI TUKUYU WILAYANI RUNGWE BAADA YA KUIBIWA WATOTO WAWILI NYAKATI MBILI TOFAUTI NA WAZAZI PAMOJA NA WANAKIJIJI WAKIHAHA KUWATAFUTA NA KUWAKUTA MAZINGIRA HATARISHI

ALEX KAPETELA  MWENYEKITI WA KITONGOJI CHA BULYAGA KATI AKIONGOZA KIKAO CHA DHARULA CHA WANANCHI WA KITONGOJI WA BULYAGA KATI ILI KUJADIRI MATUKIO YA KUIBIWA KWA WATOTO WAWILI  KWA NYAKATI TOFAUTI KATI KATIKA KITONGOJI CHA BULYAGA

WANANCHI WA KITONGOJI CHA BULYAGA KATI WAKIWA KATIKA MKUTANO WA DHARULA KUJADIRI KWA PAMOJA NA KUWEKA MIKAKATI YA KUKABILIANA NA WIZI WA WATOTO ULIOANZA KUJITOKEZA KATIKA KITONGOJI CHA BULYAGA WILAYANI RUNGWE MKOA WA MBEYA

Add caption

MHE, MWALUSAMBA DIWANI WA KATA YA BULYAGA AKIONGEA NA WANANCHI WA KITONGOJI CHA BULYAGA AMESEMA KUWA WANANCHI WANATAKIWA KUUNGANA PAMOJA NA KULAANI NA KUKEMEA HII TABIA ILIYOANZA KUJITOKEZA MAANA NI MIAKA MICHACHE ILIYOPITA AMBAPO WATOTO NANE WALIUWAWA KIKATIRI KWA KUBAKWA ,KULAWITIWA NA KUNYONGWA NA KWA MUDA MFUPI MTOTO ANAKUTWA KATUPWA POLINI

MZEE MWAIKELA AKIONGEA KWA HISIA NA KUKEMEA VIJANA KATIKA KITONGOJI CHA BULYAGA KUJISHUGHURISHA NA KUFANYA KAZI KULIKO KUPENDA PESA KWA NJIA ZA KUAMINI USHIRIKINA


Wimbi la mauwaji ya watoto wadogo laibuka upya mjini Tukuyu wilayani Rungwe baada ya tishio la kuibiwa watoto wawili katika maeneo tofauti  mjini Tukuyu wilayani Rungwe ya utatanishi huku wazazi na wanakijiji wakiwatafuta watoto hao.

Wakijadili suala hilo wananchi wa Bulyaga kati mjini Tukuyu katika kikao cha dharura kilichoandaliwa na mwenyekiti wa kitongoji cha Bulyaga kati Alex Kapetela kwa ajili ya kujadili suala hili na kupanga mikakati ya nini kifanyike ili kudhibiti kutokea tena mauaji ya watoto kama ilivotokea mwaka 2009- 2010 ambapo watoto nane chini ya miaka mitano waliuwawa kikatili kwa kubakwa,kulawitiwa na kunyongwa kasha kutupwa porini.

Wakiongea katika mkutano wa kitongoji cha Bulyaga kati wananchi  wamethibitisha kutokea kwa kitendo hicho cha kuibiwa kwa watoto na kuwa anaetumiwa kufanya uharifu huo ni mwanamke, ambaye huwalaghai watoto kwa kuwataka wampeleke sehem ambayo hujifanya yeye haifaham na wengine kuwambia waende wakawape zawadi.

Katika kikao hicho wananchi walionesha wasiwasi wao kwa serikari ya wilaya ya Rungwe kuwa wanapokamata waharifu na kuwapeleka kituo cha polisi  watuhumiwa huachiwa kwa kisingizio cha kukosa ushahidi hivyo wananchi kushindwa kutoa ushirikiano kwa kuwa watuhumiwa huwaachiwa kwa sababu ya pesa walizonazo hivyo kusita kuwataja wahusika hata kama wangekuwa wanawafahamu.

Wananchi waliomba kuwa kila mwananchi awe mlinzi wa mwenzake kwa kuangalia wageni wanaoingia na kutoka na kwamba watu wote wanaopanga kijijini hapo wajisajili kwa balozi kama ulivo utaratibu wa kitongoji cha Bulyaga kati na kushauriana wazidi kumuomba mungu kwani suala hilo linahusishwa na imani za kishirikina zaidi.

Aidha waliwataja baadhi ya watu wanaodaiwa kuhusika (majina yamehifadhiwa kwa usalama zaidi na  kukosa ushahidi) kuwa waitwe na wahojiwe na mamlaka husika lakini uongozi uliokuwepo  amesema kuwa atamuomba mwenyekiti wa kitongoji cha mpindo( wanakotokea wanaohisiwa kuwa ndio wahusika) waweze kukaa pamoja ili kupata ushahidi zaidi na maelezo ya kina kutoka kwao 

Akiongea mwenyekiti wa kitongoji cha Bulyaga kati Bwana Alex Kapetela  kuwakanya wazazi wawe wangalifu  na waache tabia ya kuwatuma watoto pekeyao dukani ama sokoni majira ya jioni.

Matukio ya kuiba watoto mjini Tukuyu wiraya ya Rungwe yaliwahi tokea mwaka 2009-2010 ambapo watoto wa kike nane wenye umri chini ya miaka mitano waliuwawa kikatili kwa kukutwa wamebakwa wamerawitiwa na kunyongwa, na kutupwa sehemu za maficho hivyo kuwapa wasiwasi kuwa yawezekana na hili likafanana na lile la mwaka huo.

TUMAIN OBEL
KINGOTANZANIA
Post a Comment