SEHEMU YA MADIWANI WA BARAZA LA HALMASHAURI YA RUNGWE |
SEHEMU YA WATENDAJI WA HALMASHAURI YA RUNGWE |
WATENDAJI WA HALMASHAURI YA RUNGWE WAKIWA MAKINI KUSIKILIZA MAELEZO YANAYOTOLEWA NA MADIWANI KUHUSU HUJUMA ZINAZOFANYIKA KATIKA MRADI WA MASOKO WILAYANI RUNGWE |
Mradi wa
maji wa masoko umeendelea kuumiza vichwa vya madiwani na watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Rungwe baada ya kesi ya jinai ya kughushi nyaraka za
bondi kuonekana kuwa na changamoto kubwa
kutokana Halmashauri ya wilaya ya
Rungwe kukosa nyaraka harisi za dhamana za mradi wa maji wa masoko hivyo
kupelekea halmashauri ya wilaya ya Rungwe kusababisha kuchelewa kukamilika kwa
mradi kwa sababu ya kuendesha kesi isiyokuwa na ushahidi huku wananchi wa
Masoko wakiendelea kukosa maji .
Akitoa
majibu ya maswali ya juu ya mradi wa maji masoko yaliyoulizwa na diwani wa kata
masukulu Mhe. Rephson Mwaisupule yaliyo ulizwa
juu ya hatua za rufaa ya kesi ya awali kushindwa na kutakiwa kulipa Tsh 786,426,316.70 pia hatima ya kesi ya
jinai ya kughushi nyaraka za bondi na
kuagiza ofisi ya mkurugenzi itafute
nyaraka husika na kuziwasilisha polisi.
Mkurugezi wa
wilaya ya Rungwe Mhe.bi Veronica Kessy amesema kwamba suala la kesi ya kughushi nyaraka ufuatiliaji
unaendelea kufanyika katika taasisi mbalimbali ikiwemo TAKUKURU, BANK na kwa
wahusika ambako nyaraka hizo zilipita mikononi mwao.
Ofisi ya
mkuu wa upererezi imesema kwamba “shauli la jinai hilo liko katika hatua za
mwisho za kiupelelezi na kinachokwamisha
ukamilishaji wake ni ofisi yako (ya mkurugenzi wa halmashauri ya wiraya
ya Rungwe) kushindwa kuwasilisha katika
ofisi hii nyaraka halisi ambazo ni Perfomance Bank Guarantee no.611512/L.32/201
ya tarehe 20.7.2010,Extension of perfamance Bond ya tarehe23.11.2011 na
Extension of performance Bank Guarantee ya tarehe 20.7.2010, nyaraka ambazo
zinatakiwa kwa ajili ya kuzipereka katika maabara ya uchunguzi wa kisayansi(FB)
Dar es salaam pamoja na sampuli za saini na sampuli za muhuri wa moto ili
zifanyiwe uchunguzi wa kitaalam”.
Ufuatiliaji
uliofanywa na Bank ya NBC makao makuu Dar es salaam wamerudisha majibu kuwa
nyaraka hizo hazipo chini ya Bank na nyaraka halisi huwa zinabaki kwa mnufaika.
Hivyo Halmashauri ya wilaya ya Rungwe imeamua kuendelea kutafuta nyaraka hizo kwa kumuandikia barua Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri
ya wilaya ya Iramba ambako John Shirima amehamishiwa na kufanya kazi huko
ambaye alikuwa ndiye mhasibu na mtunzaji wa nyaraka hizo,kupitia Mkurugenzi
wake aweze kuja kukabithi nyaraka hizo hazipo katika taarifa yake ya kukabidhi
ofisi.
Nao madiwani
wakiongozwa na diwani wa kata ya masukulu aliye pinga majibu ya Mkurugenzi, na
kusababisha mjadala mzito ndani ya kikao hicho na kumshambulia Mkurugenzi kuwa
kuna mtu anafanya kazi kwa
kumuendesha Mkurugezi na mwenywkiti nje ya vikao halali vya madiwani
na kuwa Mkurugezi ataadhimiwa na baraza na kuondoka na huyo mtu.
Wakiongea
kwa hisia kali na kuonekana kukerwa na utekelezaji mbovu wa mradi wa masoko ambao umekuwa kelo kwa wananchi kwa
mda mrefu, diwani wa kata ya Bulyaga mesema kwamba Halmashauri haina vielelezo au nyaraka hizo na wamemtaka Shirima
ashitakiwe kwa kuhusika kupoteza nyaraka makusudi na kusema kuwa kuna kundi lililofanya ubadhilifu huo ni kubwa na
wananchi wa masoko hawahitaji propaganda za kisiasa na kujinufaisha wenyewe
zaidi ya wananchi kupata maji
wanayoyasubili kwa mda mrefu bila mafanikio.
Baada ya Sakata la kukata rufaa kushindikana
kabisa baraza rimerejea ushauri wa mwana sheria wa Halmashauri ya wilaya ya
Rungwe Merick Luvinga ambapo kikao cha
awali aliishauri baraza kuwa kutokana na Halmashauri kutokuwa na nyaraka,hawawezi
kushinda kesi mahakamani hivyo aliitaka Halmashauri imlipe mkandarasi na
kufuata ushauri uliotolewa na tamisemi
waliounda kamati ya watu watano akiwemo mwanasheria na mkaguzi wa ndani wa
tamisemi baada ya kuona kuwa pande zote zinamakosa na kushauri mkandarasi wa
kwanza aendelee na shughuri hiyo ili halmashauri isije kufilisiwa na mkandalas
kutokana na pesa anazodai mkandalasi.Tsh.mil
786,426,316.70.
Kufuatia na
kuendelea kwa mgogoro huu wa utekerezaji mbovu wa mradi wa maji wa masoko,
wananchi hao kwa pamoja walipotembelewa
na kamati ya kudumu ya maji kilimo na mifugo iliyokuwa imeongozwa na Mhe. Prf Peter Kusolwa wananchi hao walieleza
kuwa hawapo tayari kushiriki kupig kura ya katiba ya maoni na uchaguzi mkuu
mwaka huu kwa kuwa ni serikari haijamilisha mradi wa maji tangu mwaka 2012 hadi
sasa wananchi wanakosa maji kwa sababu za watu wachache wasio waaminifu.
TUMAIN OBEL
KINGOTANZANIA - 0752 881456
No comments:
Post a Comment