MGENI RASMI MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CHRISPIN MEELA AKIONGEA NA WANANCHI WALIOJITOKEZA KATIKA MAADHIMISHO YA SHERIA NCHINI, AMEWATAKA WANASHERIA KUTUMIA VIZURI TAALUMA WALIYONAYO |
WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUNGWE NA WAGENI WAARIKWA WAKISIKILIZA NYIMBO KUTOKA KWA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI YA BUJINGA |
WAGENI WAARAKWA WAKISIKILIZA HOTUBA KUTOKA KWA MGENI RASMI |
WANAFUNZI WA SHURE YASEKONDARI YA BUJINGA WAKITOA BURUDANI YA MAIGIZO YENYE UJUMBE WA RUSHWA MAHARA PA KAZI |
BAADHI YA WATUMISHI WA MAHAKAMA WAKISIKILIZA HOTUBA KWA MAKINI |
PICHA YA PAMOJA YA WATUMISHI WA MAHAKAMA NA WAKUU WA TAASISI MBALIMBALI WILAYANI RUNGWE |
Wanasheria wamekuwa chanzo cha majanga na mikataba mibovu
hapa nchini kwani wao ndio wanasababisha Taifa kuingia katika mikataba
mibovu,ufisadi na chanzo cha kupoteza watumishi
wa umma wenye utendaji mzuri wa kazi.
Chrispin Meela Mkuu
wa wilaya ya Rungwe akiongea na wananchi wa wilaya ya Rungwe waliojitokeza
katika viwanja vya mahakama ya wilaya ya Rungwe katika siku ya sheria nchini,
yaliyofanyika katika viwanja vya
mahakama ya Hakimu mkazi wa wilaya ya Rungwe, yenye kauli mbiu ‘‘FURSA
YA KUPATA HAKI: WAJIBU WA SERIKALI, MAHAKAMA NA WADAU’
Mkuu wa wilaya ya
Mhe. Chrispin Meela amesema kuwa watumishi wengi wa wanasheria Tanzania waliopewa dhamana ya
kuandaa mikataba mablimbali na kusaini,hivyo kupelekea mikataba mibovu
iliyo kuwanasaini na isiyokuwa na tija
kwa taifa na kufanya vitu vya manufaa yao wenyewe sio kwa Tanzania.
Pia Chrispini Meela amewataka wanasheria kutumia taaluma yao
vizuri na kwani wao ndio wanasababisha
wananchi kuchukia serikali na chama tawala kutokana na mikataba mibovu
wanayoishauri serikali na kupoteza watumishi wazuri kwa ushauri wanaotoa.hata
hivyo ameitaka mahakama kuwa kesi zisizomaliza
upelelezi kwa mda mrefu na kwa uzembe zifutwe na atakee chelewesha kesi kwa
makusudi kwa kutoleta mashahidi mahakama wawe wakali na wamchukulie sheria kwani kuchelewesha kesi kunasababisha mahakama
ichukiwe na wananchi na ameomba mahakama za mwanzo kupunguza mashariti ya dhamana
kulingana na kesi yenyewe.
Akimkaribisha mgeni rasmi Hakimu Mkazi Mfawidhi wa wilaya ya
Rungwe Mhe. Omari Kingwele amesema ili haki iwe na maana ni razima ipatikane
kwa haki na kwa muda muafaka lakini kesi nyingi huchelewa pale mmoja wapo anaposhindwa
kutoa ushirikiano na kuwa jeshi la
polisi ndio wadau wakubwa wa mahakama kwani wao ndio wanaomkamata mharifu na
kujua ni aina gani ya ushahidi unaotakiwa
mahakamani.
Mhe. Kingwele
amesema washitakiwa wanaoachiwa huru ni kutokana na kushindwa kupata vielelezo
sahihi kutoka kwa wapelelezi na ushirikiano hafifu wa wananchi ndio unapelekea
kuachiwa huru hivyo amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwani wao ndio chanzo
cha awali kufanikisha wajibu wa haki, na kushirikiana na jeshi la polisi
kikamilifu ili kufanya kazi kwa uzuri zaidi.
Maadhimisho haya ya Sheria Wilayani Rungwe yamefanyika yakiambatana na burudani za nyimbo na maigizo kutoka shule ya Sekondari Bujinga Tukuyu mjini, yenye ujumbe wenye maudhui ya Rushwa mahara pa kazi
na wananchi walipata fursa ya kuuliza maswali kwa Taasisi zilizokuwepo za Mahakama, Jeshi la Polisi, Magereza pamoja na PCCB,na mwisho wananchi walijionea mahakama navyoendesha kesi na kujifunza
mahakama inavyofanya kazi zake za kila siku.
TUMAIN OBEL
KINGOTANZANIA
No comments:
Post a Comment