Thursday, March 12, 2015

MTAZAMO WA KIZALENDO

Wazee mkishindwa kulea na kustahimili Joto la hawa vijana mnadhani Tanzania ya kesho itaongonzwa na nani? Huu ni muda wenu wa kuwafundisha na kuwaonyesha njia sahihi (kama hawako sahihi). Leo mmeshindwa joto la Kabwe, kesho la Mnyika litawashinda, keshokutwa upande mwingine utasikia January Makamba hana nidhamu, mara Jerry Slaa naye anaendea mambo kwa pupa. utasikia Mwigulu naye hafai kuwa chamani, sasa mkiondoka nyie nani atachukua nafasi zenu?

Huwezi kuwa na zizi la Ng'ombe walio hai halafu usitegemee kukuta kinyesi zizini. Mfugaji mzuri asipokuta kinyesi zizini hujiuliza kulikoni na kumtafuta daktari wa mifugo. Tujifunze kusaafisha zizi siyo kuua au kuuza mifugo kwa kukwepa gharama ya kusafisha zizi. Inafaa tujifunze kwa ardhi jinsi inavyokubali kupasuka pindi Kiazi mbatata kinapokuwa na kupanuka. TUJIFUNZE KUISHI NA WANASIASA VIJANA AMBAO KWA KWELI NDIYO TEGEMEO LA SIASA ZETU ZA LEO NA KESHO. MNATAKA TUWE NA WANASIASA BUBU, WASIOFIKIRI, WASIOKOSOA, WASIOTAKA KUJARIBU........viongozi wa hivyo hatuwataki katika ulimwengu huu na zama hizi ambazo Nchi yetu ina Gesi, Dhahabu, Mafuta, Uranium, Tanzanite, Almasi huku tukizungukwa na watu kama Kagame, Museveni, Kenyatta, Kabila, na wale wanaotaka ziwa nyasa..halafu ndiyo mnataka tuwe na viongozi wanaokubali kila kitu bila kukosoa, kuuliza, kubisha na kuona njia mbadala. TUTUNZIENI VIJANA HAWA KWA MUSTAKABARI WENU NA WETU PIA. MKISTAAFU MTAJISIKIA FAHARI KAMA MMEACHA VYAMA VYENU NA NCHI MIKONONI MWA WATU MAKINI.
NA  Japhet Nyang'oro (fb)
........

Mtazamo wangu kuhusu hatua ya CHADEMA kumfukuza mwanachama wake Mwandamizi, Zitto Kabwe inatoa jumbe mbili kuhusu Chama hicho Kikuu cha upinzani nchini.

1. Ni chuki iliyopitiliza ya baadhi ya viongozi wa Chama hicho dhidi ya kiongozi mwenzao huyo. Hatua ya kutangaza uamuzi wa kumvua uanachama ndani ya saa moja tangu kutangazwa kufutwa kwa shauri lake, ni uthibitisho tosha wa chuki iliyopo, ni wazi CHADEMA halikuwa jukwaa salama tena kwa mwanasiasa huyo ambaye sehemu kubwa ya maisha yake ameyatumia ndani Chama hicho.

2. Kwamba, mwanachama anayekimbilia mahakamani, kupigania kile anachoamini kuwa haki yake inayogandamizwa, ni uthibitisho tosha kwamba Chama hiki hakiishi katika kile kinachodai kukipigania, DEMOKRASIA!
NA  Felix Mwakyembe (fb)
Post a Comment