Monday, April 13, 2015

MAZIKO YA WATU WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA BASI LA NGANGA YAFANYIKA HUKU WATU WANNE WAKITABULIWA NA NDUGU ZAO. 18 WALIPOTEZA MAISHA, 11 WAJERUHIWA KATIKA AJALI YA BASI LA NGANGA NA FUSO MKOANI MOROGORO







MAZIKI YAKIFANYIKA KATIKA KABURI LA PAMOJA

 

WATU 18 wamepoteza maisha papo hapo kwa kuteketea na moto huku wengine  11  wakijeruhiwa vibaya  kwa moto kufuatia magari mawili kugongana ambayo ni Basi Scania mali ya kampuni ya Nganga lililosajiliwa kwa namba T373 DAH  na gari ;la mizigo Mistubishi Fuso T164 BKG.

Ajali hiyo imeelezwa kutokea majira ya asubuhi saa mbili katika Kijiji  cha Msimba, Tarafa ya Mikumi, Wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
Polisi mkoani Morogoro kupitia kwa Kamanda wake, Leonald Paulo imesema
 chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa Basi la Nganga kuendesha gari kwa mwendo
 kasi na kulipita gari lillilo mbele yake bila kuchukua tahadhari na kusababisha  ajali hiyo.
Kamanda Paulo aksema basi lilikuwa limepakia pikipiki katika buti na ambayo ilikuwa na mafuta hivyo baada ya kugongana palitokea mlipuko na kusababisha moto mkubwa ulioteketeza basin a lori hilo.

Mbali na abiria waliokufa ni madereva wa magari yote mawili walioteketea kabisa na moto huo na abiria walioshindwa kujiokoa na majeruhi takribani 11 walikimbizwa katika Hospitali ya Mtakatifu Kizzito  Mikumi.

No comments: