Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali kutoka Makao makuu, Dk. Magreth Mhando akikata utepe kuzindua mnara wa upasuji wa tundu dogo (LAPARASCOPIC TOWER) |
Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali kutoka Makao makuu, Dk. Magreth Mhando akiongea na watumishi na wageni waalikwa mara baada ya kuzindua mnara wa upauaji katika Hospitali ya Rufaa Mbeya |
Mkurugenzi wa Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Nyanda za juu kusini, Dk.Mpoki Ulisubisya, akisoma taarifa fupi mbele ya mgeni rasmi |
Fedric Ogumbo mkurugenzi wa kampuni ya Baylem kutoka Kenya ambaye ametoa msaada wa vifaa vya upasuaji vyenye thamani ya zaidi ya dola za kimarekani 5000. |
Baadhi ya Madkatari na wauguzi wakimsikiliza mgeni rasmi kwa makini |
Dr. Lazaro Mboma mkuu wa idara ya upasuaji na Daktari bingwa upasuaji akimwelezea mgeni rasmi jinsi mnara wa upasuaji unavyofanya kazi |
Moja ya aliyetengeneza mtambo wenyewe wa upasuaji kwa njia ya tundu dogo kutoka Kampuni ya Gimmi ya Tutlingen nchini Ujerumani mkono wa kulia akielezea jinsi mtambo huo unavyofanya kazi |
| |
HOSPITALI ya Kanda ya Rufaa ya Nyanda za juu kusini-
Mbeya, imezindua mnara wa upasuaji wa tundu dogo(LAPARASCOPIC TOWER) utakaopunguza
wagonjwa kuomba Rufaa ya kwenda kutibiwa katika hospitali zingine.
Akizungumza katika uzinduzi huo
, Mkurugenzi wa Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Nyanda za juu kusini, Dk.Mpoki
Ulisubisya, alisema msaada huo utapuguza idadi ya wagonjwa ambao wamekuwa
wakiomba rufaa pia hitaji halisi la Hospitali hiyo la ufinyu wa nafasi ya
kulaza wagonjwa na kupunguza msongamano wa wagonjwa.
Alisema kutokana na changamoto
hizo uongozi wa Hospitali ulifikiria namna ya kusogeza huduma ya upasuaji kwa
njia ya Tundu dogo kwa Wagojwa ambapo ulishirikiana na wadau mbali mbali ili
kufanikisha hilo na baadhi yao kuitikia na hatimaye kukubali kulitekeleza.
Aliwataja baadhi ya marafiki
walioitikia wito huo na kuliwezesha suala hilo kufanikiwa kuwa ni pamoja na
John Fedric Ogumbo ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Baylem kutoka Kenya
ambaye alitoa msaada wa vifaa vya upasuaji vyenye thamani ya zaidi ya dola za
kimarekani 5000.
Aliongeza kuwa Kampuni hiyo pia
imesaidia Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kufadhili mafunzo kwa madaktari wanne
nchini Ureno kwa gharama isiyopungua Euro 24000 hali iliyochangia Hospitali
hiyo kuwa na watalaamu waliobobea kuliko Hospitali zingine nchini.
Mkurugenzi
huyo alisema mtu
mwingine wa kumshukuru ni aliyetengeneza mtambo wenyewe wa upasuaji kwa
njia ya tundu dogo kutoka Kampuni ya Gimmi ya Tutlingen nchini
Ujerumani ambao wameahidi kuhakikisha madaktari
waliosomea watafanyakazi kwa weledi na ufanisi.
Alizitaja kazi za mtambo huo
kuwa ni pamoja na upasuaji wa mawe kwenye njia ya nyongo, upasuaji wa kidole
tumbo, upasuaji wa Tezi dume na upasuaji wa magonjwa ya akina mama.
Alisema faida ya mtambo huo ni
pamoja na upasuaji kufanyika kwa muda mfupi tofauti na uliozoeleka, ufupi wa
mgonjwa kukaa hospitalini, maumivu kidogoukilingianishwa na upasuaji mkubwa kwa
njia ya visu na kuzuia damu nyingi kupotea wakati wa zoezi la upasuaji.
Kwa upande wake Mgeni rasmi
katika uzinduzi huo ambaye ni Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali kutoka Makao makuu,
Dk. Magreth Mhando alisema Wizara ya afya kupitia Sera ya Afya na mpango wa
maendeleo ya afya ya msingi, sekta ya msingi na zinginezo inakusudia kuboresha
mazingira ya sekta hiyo.
Alisema Serikali inaipongeza
Hospitali hiyo kwa juhudi ambazo inaendelea kuzifanya ambazo ni kuwa na majengo mazuri, stahiki za watumishi, vitendea
kazi, utawala bora na kumjali mteja jambo ambalo linaifanya Hospitali hiyo
kuzidi kuwa bora na kuwa mfano wa kuigwa.
Aidha alitoa pongezi kwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuiinginza Sekta ya afya katika matokeo
makubwa sasa(BRN)unaoanza kutkelezwa katika awamu ya pili ukijikita katika
sehemu nne.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment