Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva (wa pili kulia) akizungumza
na waandishi wa habari wakati akitangaza majimbo mapya ya uchaguzi
katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam leo. (Picha na
Emmanuel Massaka Globu ya Jamii)
………………………………………………..
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza majimbo 26 mapya ya
uchaguzi ambayo yatakuwa na wagombea katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika
Oktoba 25 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari
leo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian
Lubuva amesema kukata kwa majimbo hayo wamezingatia idadi ya watu pamoja
na Jiografia katika majimbo mapya.
Amesema katika upande wa Zanzibar majimbo yamebaki kuwa 50 kama awali hiyo inatokana vigezo vilivyowekwa na tume hiyo.
Majimbo yaliongezwa ni Handeni Mjini, Nanyamba, Makambako,
Butiama, Tarime Mjini, Tunduma, Msimbo, Kavu, Geita Mjini, Mafinga
Mjini, Ushetu, Nzega Mjini, Kahama Mjini, Kondoa Mjini, Newala Mjini,
Bunda Mjini, Mbulu Mjini, Ndanda, Madaba, Mbinga Mjini, Mbagala,
Kibamba,Vwawa,Monongo,Mlimba, Pamoja na Uliambulu.Amesema katika upande wa Zanzibar majimbo yamebaki kuwa 50 kama awali hiyo inatokana vigezo vilivyowekwa na tume hiyo.
Jaji Lubuva amesema baadhi ya wabunge wamekuwa wakiingia katika Halmashauri mbili hiyo kuweka mipaka katika maeneo ili mbunge aweze kushiriki katika Halmashauri moja tu.
Amesema baadhi majimbo yamebadilishwa majina na kuendelea kuwepo kwa majimbo hayo kisheria.
No comments:
Post a Comment