Monday, September 21, 2015

DR.JOHN POMBE MAGUFULI: SITAKUA DIKTETA NITAFUATA UTAWALA WA SHERIA NA KUWA KIONGOZI WA WATETEZI WA WANYONGE

001
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akihutubia mkutano wake wa kampeni kwenye uwanja wa Chato wialayani Chato mkoani Geita ambapo amewaomba wananchi wa Chato ambako ndiko alikozaliwa kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani.
Dk. Magufuli amesema mara atakapochaguliwa serikali yake itakuwa ni ya Watazania wote bila kujali vyama vyao, Dini zao, Makabila yao wala Itikadi zao atakuwa rais wa watanzania wote na lengo lake kubwa ni kuwatumikia watanzania na kuangalia zaidi na kuboresha hali za watanzania masikini ili nao waweze kukua kiuchumi.
Dk. Magufuli amesema kuna watu wameanza kuwatisha wananchi kwamba yeye ni mkali, Amesema "Si kweli yeye ni mpole sana ila nikiwa madarakani nitaongoza nchi kwa utawala wa sheria na kuwapa haki watanzania kulingana na sheria za nchi zanavyoelekeza kuendesha nchi hivyo sitakuwa kiongozi dikteta kama wanavyofikiri wengine". Japokuwa ninauchukia uzembe kazini, Wizi na ufisadi.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-CHATO)
1
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akihutubia mkutano huo mjini Chato leo.
3
4
Picha mbalimbali zikionyesha umati wa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.(P.T)
5
6
7
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akiserebeka na msanii Chege wa kundi la TMK Wanaume wakati lilipokuwa likitumbuiza katika mkutano huo.
9
Wasanii Mh. Temba kulia na Chege kutoka TMK Wanaume wakitumbuiza katika mkutano huo.
10
Msanii Shilole naye akasuuza nyoyo za wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.
11 12
Kundi la TOT likitumbuiza kwenye mkutano huo
006
Mke wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiwasalimia wana Chato na kumuombea kura mumewe pamoja na wabunge wa CCMna Madiwani.
13
Mke wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiwa amekaa na Mkuu wa mkoa wa Geita Mh. Fatma Mwasa kushoto wakiwa katika mkutano huo.
14
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza katika mkutano huo.
15
16
Msanii Mr Blue akifanya vitu vyake jukwaani.
17
Kundi la Orijino Kemodi wakionyesha vichekesho vyao jukwaani.
18
Yamoto Band wakifanya vitu vyao jukwani.
19 21
Ali Tumbo akapanda jukwaani na Mbuzi akisakata muziki ili mradi burudani tu.
22
Malkia wa Mipasha Khadija Omar Kopa wa TOT akitumbuiza katika mkutano huo.
23
Msanii Fid Q naye akaghani kwa mistari yake migumu ya Ki -HipHop na kushangiliwa vya kutosha.
24
Mwanamuziki Bushoke akiiba wimbo wake katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi ilani ya uchaguzi Dk. Merdad Kalemani mgombea ubunge wa jimbo la Chato baada ya kumpigia debe.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akiwapigia debe wagombea ubunge wa mkoa wa Geita kutoka kulia ni Vick Kamata mgombea wa viti maalum mkoa wa Geita na Joseph Kasheku Msukuma mgombea ubunge wa jimbo la Geita vijijini.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akiondoka kwenye mkutano mara baada ya kuhutubia mkutano wa kampeni mjini Chato leo.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
30
Msafara wa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli ukiondoka kuelekea nyumbani mara baada ya mkutano huo.
Post a Comment