Sehemu ya mabasi 138 ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) yaliyowasili katika Bandari ya Dar es Salaam, kwa ajili ya kuanza kutoa huduma ya usafiri katika kipindi cha mpito kwenye miundombino ya mfumo wa mabasi yaendayo haraka (BRT)kuanzaia mwezi ujao.
Mkuu wa
Mkowa Dar es Salaam, Bw. Saidi Meck Sadiki akijaribu basi la Mradi wa
Mbasi Yaendayo Haraka (DART), alipofanya ziara katika Bandari ya Dar es
Salaam kujionea kuwasili kwa Mabasi 138 ya Mradi huo ambayo mwezi ujao
yataanza kutoa huduma ya usafiri jijini Dar es Salaam katika Kipindi cha
mpito.
Mkuu wa
Mkowa Dar es Salaam, Bw. Saidi Meck Sadiki akishuka katika basi la Mradi
wa Mbasi Yaendayo Haraka (DART), alipofanya ziara katika Bandari ya Dar
es Salaam kujionea kuwasili kwa Mabasi 138 ya Mradi huo ambayo mwezi
ujao yataanza kutoa huduma ya usafiri jijini Dar es Salaam katika
kipindi cha mpito.Mabasi 138 ya Mwendo Kasi (BRT), yamewasili katika
Bandari ya Dar es Salaam kutoka nchini China. Kuwasili kwa mabasi hayo
kutasaidia kupunguza tatizo la usafiri katika Jiji la Dar es Salaam.
Katika
Bandari ya Dar es Salaam kutoka China tayari kwa huduma ya usafiri.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, aliwaambia waandishi
wa habari jana baada ya kufanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam
kujionea kuwasili kwa mabasi hayo.
“Tumefikia
hatua nzuri na naipongeza Kampuni ya Uda Rapid Transit (Uda-RT) kwa
kuleta mabasi hayo kwa ajili ya kuanza kutoa huduma hii ya usafiri
katika kipindi cha mpito. Hii itasaidia kuondoa adha ya usafiri kwa
wakazi wa jiji hili,” alisema.
Alisema
serikali ilifanya kazi kubwa kuunganisha Kampuni ya Usafiri Dar es
Salaam na wamiliki wa daladala na baadaye kuanzisha kampuni ya Uda-RT.
Hata hivyo, alisema taarifa za nauli za mabasi hayo ya Sh. 900 zilizotolewa katika mtandano, zilikuwa ni uzushi na upotoshaji.
Alisema
suala la nauli linahusisha ushiriki wa taasisi mbalimbali chini ya
Mamlaka ya Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) na hivyo uzushi
huo umewaletea usumbufu mkubwa wakazi wa Dar es Salaam hivyo wanatakiwa
kuwapuuzia.
Msemaji
wa Kampuni ya Uda-RT, Subri Maburuki, alisema mabasi yote yameingia
yakiwamo ya mita 12 yapo 101 na mita 18 yapo 39 na huduma ya usafiri
kipindi cha mpito kitaanza baada ya kukamilisha taratibu za bandari.
“Tuliahidi
kuwa mwezi huu mabasi yatakuwa yamewasili na ni kweli yamekuja, kwa
pamoja na yale ya kufundishi yatakuwa mabasi 140,” alifafanua Maburuki.
Kaimu
Meneja Bandari ya Dar es Salaam, Hebel Mhanga, alisema meli iliyobeba
mabasi hayo ilipitia Kenya na kimsingi kutokea nchini China, ilikuwa
imebeba magari 1,700 yakiwamo mabasi ya Uda-RT.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment