MJUMBE wa
Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) na Mbunge wa Urambo aliyemaliza muda wake,
Samuel Sitta ametaka uandaliwe mdahalo kwenye vyombo vya habari kati
yake na mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa uelezwe ukweli juu ya
ukweli wa sakata la Richmond.
Sitta
ambaye alikuwa Spika wa Bunge wakati Lowassa alipojiuzulu kutokana na
sakata hilo, alisema katika mdahalo huo, ataeleza ukweli juu ya uhusika
wa Lowassa katika sakata hilo na atatoa vielelezo kueleza taifa ufisadi
uliokuwa ukifanyika.
Alisema
hayo jana kwenye ufunguzi wa kampeni za CCM mkoa wa Shinyanga katika
mkutano uliofanyika mjini hapa ambao wagombea wa udiwani na ubunge wa
majimbo yote ya mkoani hapa walitambulishwa.
Katika
mkutano huo, alisema kujiuzulu kwa Lowassa mwaka 2008, kulitokana na
Kamati Teule iliyoongozwa na Dk Harrison Mwakyembe, kugundua kwamba
fedha za walipa kodi zilikuwa zikipotea bure.
Alisema
yuko tayari kusimulia kwa umma utajiri wa mgombea huyo wa Chadema.
Makundi, urafiki Sitta ambaye ni Waziri wa Afrika Mashariki, ambaye pia
alikuwa kwenye kinyang’anyiro cha kutaka kuteuliwa kugombea urais
kupitia CCM, alisema wanamwamini Dk John Magufuli katika utendaji wake
wa kazi na pia ni kiongozi asiye na makundi au urafiki.
“Kweli
lazima uwapime viongozi, kwani anayetaka urais lazima achaguliwe kwa
kufuata utaratibu, achambuliwe usiogope moshi kama unapikia
kuni...lakini mwenzetu Lowassa hakukubaliana na hayo, akaona kaonewa kwa
madai anafaa kuwa rais mbona sisi tulikubali?,” alihoji Sitta.
Aliendelea
kusema, “hali hiyo, ilionesha ndani ya CCM kulikuwa na vyama viwili
ambavyo ni ‘CCM Katiba’ na ‘CCM Maslahi’ ambayo alikuwa anaongoza
Lowassa na mfuasi wake, Mgeja (aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Shinyanga ambaye pia alihamia Chadema hivi karibuni).
”
Wanachama
mapandikizi Sitta alisema CCM ilikuwa imejaa wanachama walio
mapandikizi tofauti na sasa ambapo alidai wamekwisha jionesha na
kimekuwa chama kizuri kama ilivyokuwa enzi za hayati Baba wa Taifa,
Mwalimu Julius Nyerere.
Alisisitiza
kwamba kitazidi kuimarika na waliobaki wataendelea kutetea ilani na
kuhakikisha chama kinaendelea kushika dola. Kwa mujibu wa Sitta, wakati
wa mchakato, baada ya kumaliza vikao, Lowassa alikuwa akiitisha vikao
vya kundi lake alilolibatiza CCM Maslahi na kuwaagiza wapambe wake
kuitisha vyombo vya habari kushambulia watu ambao hawako kwenye mlengo
wao.
Wakati
huo huo mjumbe huyo wa NEC, alikumbusha umati uliohudhuria mkutano huo
kwamba, uchaguzi wa mwaka huu unatumia Katiba ya zamani ya mwaka 1977
ambayo inatamka matokeo ya rais hayahojiwi hata kama aliyeshinda,
amezidi kura moja.
Sitta
ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, alisema alishauri wabunge
wasitoke nje ya Bunge hilo waweze kutumia katiba hiyo iliyokuwa na
kipengele cha kuhoji matokeo ya rais sasa imekula kwao.
Lusinde ahoji
Kwa
upande wake, Mbunge wa Mtera, ambaye pia mjumbe katika kampeni ya
uchaguzi Livingstone Lusinde , alihoji sababu za Lowassa kulalamikia
kukatwa akisema ameonewa. “Mbona kaingia Chadema siku moja, ya pili
kaingia kwenye nafasi ya urais; mbona na yeye huko kawaonea wenzake
aliowakuta,” alihoji Lusinde.
Wanaomtumia Nyerere
Aliyewania
ubunge kupitia kura za maoni ndani ya chama, jimbo la Shinyanga Mjini ,
Hassan Athumani alieleza kushangazwa na wanaogeuza kauli ya Baba wa
Taifa, Nyerere kwa kuleta maudhui tofauti juu ya dhana ya mageuzi.
Alisema
kauli ya Nyerere kwamba Watanzania wakikosa mageuzi ndani ya CCM
watayapata nje ya CCM, hakuwa na maana kama inavyofikiriwa na waliohama
chama kwamba wakikosa udiwani, ubunge na urais, waende upinzani.
UVCCM na Richmond
Wakati
huo huo Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka katika taarifa
yake kwa vyombo vya habari, alisema wameshangazwa kuona mgombea wa
Chadema, Lowassa akishindwa kuzungumzia ufisadi, kutaja walioshindwa
kuwajibika, kukiuka maadili ya uongozi wakiwamo wa sakata la Richmond.
“Tumeshangaa
kumuona akishindwa kuzungumzia masuala ya ufisadi na kutowataja wezi
waliopora rasilimali za umma na maliasili za nchi, waliofuja uchumi,
wala rushwa, watu waliokosa kuwajibika na kutochukuliwa hatua za
kisheria kwa masuala mazima ya kukiuka maadili ya uongozi ikiwemo sakata
zito la mradi wa kufua umeme wa dharura kupitia kampuni hewa ya
Richmond,” alisema.
HABARI LEO
No comments:
Post a Comment